Kikosi kamili cha Yanga kilichoifunga Azam FC 3-0 katika mchezo wa Ngao ya jamii hii leo.
Kikosi cha Azam FC.
Mshambuliaji Geilson Santos Santana “Jaja” raia wa Brazil leo ameiwezesha timu yake ya Yanga kutwaa ngao ya Jamii katika ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Azam FC huku yeye akitumia magoli mawili ya mwanzo na Saimon Msuva.
Yanga ikicheza chini ya Kocha Mbrazili Marxio Maximo wamepata ushindi huo ikiwa ni ishara njema kwa mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara kwa msimu mpya wa ligi unaoanza Septemba 20.
Ushindi huo ni salamu kwa Mtibwa Suger ambayo ndio watafungua nao ligi Kuu huko Morogoro uwanja wa Jamhuri.
BONYEZA HAYA MANENO "U LIKE PAGE YETU"TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU ZINAPOTOKEA
BONYEZA HAYA MANENO "U LIKE PAGE YETU"TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU ZINAPOTOKEA
Social Plugin