Binti
mdogo wa miaka 15 raia wa Argentina Julia Alvarez amepatwa na majanga
yaliyomfanya apoteze muonekano wake mzuri baada ya mabinti wawili wenye
wivu kumcharanga uso wake kwa visu kisa uzuri wake uliopitiliza!
Julia anasema alikuwa anatembea kurudi nyumbani akitokea mji wa Juan
Domingo Peron huko northern Argentinian ndipo wasichana hao wawili mmoja
ana miaka 18 na mwingine 16 walipomvaa bila huruma.
"Kila mtu anasema wewe ni mzuri sana..huwezi kuonekena mzuri tena
tukishamalizana na wewe hapa..na watu watakuita majina mabaya'' Julia
alisema haya ni maneno aliyoambiwa kabla ya kucharangwa visu usoni.
Hili ni eneo ambalo tukio hilo la kikatili lilipofanyika .
Kupitia ukurasa wa facebook dada wa Julia aliandika ;
"Walikuwa wanamuonea wivu sana mdogo wangu na kila mara wamekuwa
wakimsumbua lakini sikutegemea kama wangefika mbali kiasi hiki.
Nimejaribu kuwa imara lakini kila muda namuona mdogo wangu nataka kudondosha machozii...wamemuharibia maisha. Anasema anataka kujiua kwa sababu kila akijitizama kwenye kioo anajiona mbaya sana sasa, wameharibu familia yetu''

Polisi waliwatia mbaroni mabinti hao lakini walimuachia wa miaka 16 kutokana na umri wake ila wa miaka 18 bado wamemshikilia.
Social Plugin