Angel di Maria akiwa na tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba wa
Manchester United,.KIUNGO mshambuliaji wa Manchester United, Angel di
Maria ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba klabuni hapo.
Di Maria kazini.Di Maria ametwaa tuzo hiyo baada ya kupata 68% ya
kura zote zilizopigwa kupitia tovuti ya ManUtd.com, huku nafasi ya pili
ikienda kwa Ander Herrera aliyepata 23% huku Rafael akiambulia 9% ya
kura hizo.
Staa huyo raia wa Argentina amesema anafurahi kuona ameanza vizuri
maisha yake ndani ya Manchester United na anamatumaini kuwa
anachokifanya uwanjani kinaisaidia timu kupata ushindi na poniti.
Social Plugin