Mwili wa aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Athuman Livigha ukiwasili nyumbani kwake Bunju jijini Dar leo.
Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala (wa pili kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe (wa tatu kushoto) msibani kwa Profesa Athuman.
Mwili wa Profesa Athuman ukiingizwa nyumbani kwake Bunju, Dar.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu.
Mwili wa marehemu ukiombewa kabla ya maziko.
Mwili wa Profesa Athuman Livigha ukipelekwa makaburini kwa maziko.
Mwili wa aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Athuman Livigha, aliyefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi nyumbani kwake, Bunju jijini Dar es Salaam umezikwa leo.
Marehemu aliuawa uSeptemba 30, mwaka huu majira ya saa 3 usiku akiwa nyumbani kwake. (PICHA: MAKONGORO OGING' NA HARUNI SANCHAWA / GPL)
Social Plugin