Askari polisi wakichukua mwili wa marehemu kutoka ndani ya chumba-Picha na Marco Maduhu/Agnes Kambarage-Malunde1 blog
Mwili wa marehemu ukichukuliwa na polisi-Picha na Marco Maduhu/Agnes Kambarage-Malunde1 blog
Polisi wakiondoka na mwili wa marehemu-Picha na Marco Maduhu/Agnes Kambarage-Malunde1 blog |
Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya gari la polisi-Picha na Marco Maduhu/Agnes Kambarage-Malunde1 blog
Kijana
Mmoja aliyefahamika kwa jina la Rajabu Issa (36), mkurya mkazi wa Majengo mjini Shinyanga mkoani
Shinyanga, hatimaye ametimiza lengo lake la kujinyonga baada ya kuwa akimwambia
mke wake ipo siku atajiua.
Tukio
hilo limetokea jana asubuhi huku chanzo cha kifo cha kijana huyo kikiwa
hakijulikani.
Akizungumza
na Malunde1 blog ,mke wa marehemu bi Mgeni Hamis (23), alieleza kusikitishwa na
kifo cha mme wake na kusema kuwa enzi za uhai wake alikuwa na tabia ya
kumuambia mara kwa mara mkewe, kama utani kuwa ipo siku atajiua lakini kila akimuulizia
sababu za kujiua nini ,alikuwa hamwambii na kumpa jibu kwamba hata akimwambia
huwezi kumuelewa.
Mgeni
alisema siku ya jana ambapo tukio hilo lilimetokea, ilipofika majira ya saa
tatu asubuhi, Marehemu alimwambia mke wake kuwa aende kwao mtaa wa Ngokolo
mjini hapa, akamsalimie mama yake mzazi (Mama yake na mwanamke),kutokana na
mama huyo kuwa mgonjwa.
“Tumeamka
vizuri na mme wangu, na ilipofika majira ya saa tatu asubuhi akaniambia niende
nyumbani kwetu nika msalimiae mama yangu mzazi kwa vile ni mgonjwa, ndipo
nikaondoka ,lakini baada ya masaa
machache, nikapigiwa simu na shemeji yangu wa Musoma kuwa mme wako mbona
anatutumia meseji za vitisho, kuna nini huko?,”
“Ndipo
nikaamua kumpigia simu mme wangu, ambapo iliita bila ya kupokelewa, nikachukua
jukumu la kumpigia mpangaji mwenzangu ,Idaya Ibrahimu, akamwangalie mme wangu
ndani mbona hapokei simu”
“ Alipoingia
ndani kwangu ndipo akamkuta mme wangu kajinyonga juu ya dali, na amefariki
dunia” alieleza mke wa marehemu.
Akielezea
tukio hilo zaidi mpangaji mwenzake Idaya Ibrahimu, alisema baada ya kupigiwa
simu hiyo majira ya saa tano asubuhi na mkwe wa marehemu, kwenda kumuangalia
mme wake kama yumo ndani, ndipo alipomkuta kaning’inia juu ya dali akiwa na
kamba shingoni na amesha poteza maisha.
Alisema
baada ya kuona tukio hilo, ndipo alipochukua jukumu la kumtaarifu mke wa
marehemu, majirani wenzake, pamoja na jeshi la polisi, ambalo lilifika na
kuuchukua mwili huo, na kuupeleka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kwenye
hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga SACP Justus Kamugisha amethibitisha
kutokea kwa kifo cha kijana huyo, na kusema kuwa hakuna mtu yeyote
anayeshikiliwa na jeshi la polisi juu ya kifo hicho, na uchunguzi bado
unaendelea ili kubaini chanzo chake.
Habari
imeandaliwa na Marco Maduhu-Malunde1 blog-Shinyanga
Social Plugin