Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA_MAUAJI YA KUTISHA KANISANI HUKO BUKOBA


Katika hali isiyo ya kawaida,watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana wamevamia Kanisa la PAG tawi la Kagemu kata ya Kitendaguro manispaa ya Bukoba na kumua muumini mmoja kwa kumcharanga mapanga hadi kufa na mwenzake kujeruhiwa, hawakuiba chochote ikiwemo simu zao.

Hata hivyo tukio hilo linahusishwa na imani za kidini kwamba waliohusika na tukio hilo ni wapinzani ya dini yao.

Mtoa habari aliyegoma kutaja jina amesema chanzo cha mgogoro huo na kifo cha muumini ambaye ni mwalimu katika shule ya sekondari KAGEMU ni baada ya marehemu kuoa mwanamke wa dini nyingine (inaifadhiwa) na kumbadilisha dini huyo mkewe na hapo waumini wa dini ya mkewe walianza vitimbwi kwa kanisa hilo na hadi mauaji hayo kumekuwa na vurugu za kila mara baina ya pande mbili. 

Polisi bado wanachunguza na watatoa taarifa baadae,mwili wa marehemu umeifadhiwa katika chumba cha maiti bukoba mjini,majeruhi amelazwa hospital ya mkoa. 
Viongozi wa makanisa ya PAG walitarajiwa kutoa tamko rasmi jana.


Bonyeza Maneno haya Tukutumie Habari zetu zote moja kwa moja hapo ulipo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com