Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA 20_MAZISHI YA MSANII WA TMK WANAUME FAMILY ,YP LEO JIJINI DAR ES SALAAM


Waombolezaji wakiwa wamebeba bango lenye picha ya marehemu.


 Marehemu Yesaya Ambikile Mwakalekamo  'YP' amezikwa hii leo katika makaburi ya Changombe jijini Dar es salaam.
Marehemu YP alifariki jana baada ya kuugua kifua na kulazwa katika Hospitali ya Temeke hadi mauti yalipo mkuta.

Awali kabla ya maziko hayo YP aliagwa na ndugu jamaa na marafiki zake katika viwanja vya sigara Chang'ombe ambapo wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongo fleva na Bongo muvi walihudhuria.
Wasanii wa Bongo Fleva wakiuaga mwili wa marehemu Yesaya Ambikile 'YP' katika Viwanja vya TCC Chang'ombe, Dar es Salaam.
 YP kabla ya kuhamia katika sanaa ya uimbaji na kuibuka na kundi la wanaume Family alikuwa akifanya sanaa ya maigizo na vichekesho akiwa kundi moja na wasanii, Masanja Mkandamizaji, Mpigapicha maarufu na Blogger Mroki Mroki, Kiwewe, Dokii enzi hizo wakiwa na kundi la Get Well Generation lililokuwa chini ya Dokii na kurusha michezo yake Star Tv.

Mke wa marehemu YP, Sakina Robert (mwenye kiremba cheupe) akiwa katika hali ya majonzi.
YP enzi za uhai wake alitamba na nyimbo kama 'Ulipenda Pesa', 'Pumzika', 'Shemsha' na nyimbo nyingi za TMK Wanaume Family kama 'Twende zetu' ya Chege, 'Dar mpaka Moro', 'Kichwa kinauma', 'Tufurahi' na nyimbo nyingi za TMK Wanaume family pia alivuma na wimbo wa Binadamu Visa alioimba na swahiba wake, Y-Dash.
Wasanii wa Bongo Fleva wakiuaga mwili wa marehemu Yesaya Ambikile 'YP' katika Viwanja vya TCC Chang'ombe, Dar es Salaam.

 Kiongozi wa kundi la Yamoto Band na TMK, Mkubwa na Wanawe, Saidi Fela akizungumza wakati wa msiba huo. 
Msanii wa Bongo Fleva, Juma Nature akizungumza jambo kwa niaba ya wasanii wenzake waliofanya kazi na marehemu enzi za uhai wake.

 Mh Temba nae akizungumza...
 Mmoja wa waigizaji aliyehudhuria mazishi hayo, Jacob Steven 'JB' akizungumza.
Ilikuwa ni vilio kutoka kwa kila mtu aliyehudhuria mazishi hayo



Juma Nature akifunua jeneza tayari kwa shughuli ya kuuaga mwili huo.

Mtoto wa marehemu, Ambikile Yesaya akisogezwa mbele ye jeneza kuuaga mwili wa baba yake.

Msanii wa filamu, William Mtitu akipita kuaga mwili wa marehemu.

Msanii wa vichekesho, Mussa Kitale 'Mkude Simba' akiaga mwili.

Waombolezaji wakiwa katika msiba wa msanii wa Bongo Fleva, Yesaya Ambikile 'YP' kwenye Viwanj vya TCC, Chang'ombe, Dar.

Jeneza likishushwa kaburini.



Sehemu ya mamia ya waombolezaji wakiwa makaburini.



PICHA KWA HISANI YA WADAU MBALIMBALI WA MALUNDE1 BLOG,WALIOKUWA ENEO LA TUKIO LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Malunde1 blog,inawapa pole ndugu,jamaa na marafiki wote waliofikwa na msiba huu.Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu YP.Amina!!

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com