Wadau wa elimu wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika mkutano huo.Mada mbalimbali zilitolewa kama vile kukumbushwa na kuhimizwa kutimiza wajibu wao,haki zao za msingi katika utumishi na jinsi ya kuzidai kwa mujibu wa sheria na kanuni na taratibu za kazi
Afisa elimu mkoa wa Shinyanga Eva Lopa akizungumza katika mkutano huo leo
Katibu wa CWT mkoa wa Shinyanga mwalimu Rehema Sitta akizungumza katika mkutano huo leo ambapo aliwataka walimu wenzake kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi
Walimu pia walisisitizwa kujenga tabia ya kupenda kujisomea nyaraka mbalimbali ili kuongeza maarifa na ufahamu wa vitu mbalimbali
Naibu katibu mkuu wa CWT nchini mwalimu Ezekieh Oluoch akitoa mada juu ya uendeshaji na usimamizi wa vyama vya wafanyakazi nchini
Mkutano unaendelea
Naibu katibu mkuu wa CWT nchini mwalimu Ezekieh Oluoch akizungumza katika mkutano huo,kulia kwake ni mwenyekiti wa CWT mkoa wa Shinyanga Endrew Nyanguzu,wa kwanza kulia ni katibu wa CWT mkoa wa Shinyanga Rehema Sitta,wa pili kutoka kulia ni afisa elimu mkoa wa Shinyanga Eva Lopa
Mkutano unaendelea
Mwenyekiti wa CWT mkoa wa Shinyanga Endrew Nyanguzu akizungumza katika mkutano huo wa wadau wa elimu mkoa wa Shinyanga leo |
Meneja utawala kutoka mfuko wa pensheni wa PSPF Neema Kuwite akitoa mada kuhusu mfuko wa hifadhi ya jamii PSPF |
Mkutano unaendelea |
Katibu tawala wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi alichangia mawili matatu katika mkutano huo wa wadau wa elimu |
Wadau hao wa elimu walizitaja changamoto zinazowakabili walimu mkoani Shinyanga kuwa ni mitihani ya Mock darasa la saba kusahihishwa na wanafunzi na maafisa elimu kuona kuwa vikao vya walimu na CWT vinapoteza vipindi
Changamoto nyingine iliyoibuliwa ni ile ya baadhi ya wakuu wa idara(maafisa elimu,maafisa utumishi na wahudumu wa ofisi kutukana walimu
Viongozi wa Chama cha Walimu waliwaomba watoa huduma katika halmashauri zote watoe ushirikiano kwa CWT na kwa walimu ili lengo la kuboresha elimu liweze kufanikiwa.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga
Social Plugin