Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa akizungumza jambo.
“Hakuna ndoa kati ya mtu yeyote ambaye amezidi miezi 6 bila kukutana na
mumewe kwa mujibu wa dini ya kiislamu.
SHEIKH Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa ameweka wazi kuwa
msanii nyota wa filamu, Aunt Ezekiel ambaye aliolewa na Sunday Demonte
hana ndoa kutokana na kukaa mbali na mumewe kwa zaidi ya miezi sita.
Kwa
kawaida mwanamke ambaye hajakutana na mumewe kwa miezi 6 au zaidi baada
ya ndoa yao, hupaswa kwenda mara moja Baraza Kuu la Waislamu Tanzania
(Bakwata) kulalamika na hatimaye kudai talaka, ikiwa mwanamke ameridhika
na hali hiyo, naye akaamua kukaa kimya huku akifanya mambo yake na
kuanzisha uhusiano na wanaume wengine maana yake amejitoa mwenyewe
kwenye mamlaka ya mumewe, hivyo hapo kunakuwa hakuna ndoa tena,”alisema
Shehe.
Social Plugin