Lile kundi la Hiphop lilikua linaundwa na Heavy Weight MC, Profesa
Jay, Big Wille pamoja na Fanani, "Hard Blasters" ambao walikua active
kuanzia miaka ya tisini hadi miaka ya 2000 mwanzoni, baada ya kuachia
album iliyokuwa na ngoma kali na hit kama chemsha bongo na niamini, na
kupotea kwenye ramani baada ya hapo,
sasa kundi hilo (HBC) linatarajiwa kurudi tena kwenye ramani ya bongo
fleva chini ya studio za Mwanalizombe zinazomilikiwa na Prof Jay.
"Hard Blasters kipindi kirefu, kila mtu aliamua kuishi maisha yake, mi
nilipoamua kuwamba kufanya solo project kwasababu wenzangu waliokuwa
slow kidogo, na mimi kwasababu niliamua muziki uwe maisha yangu, ndio
kazi yangu na ndio maana niliacha kazi niliyoajiriwa ili nifanye mziki,
ilibidi niendelee kufanya mziki, nilishindwa kuwasubiri wenzangu, lakini
kwasababu wako tayari na wako pamoja na bado tunaishi pamoja, kila siku
ilikuwa nikiwauliza lini wanaweza wakawa tayari wanasema tutafanya
tutafanya tutafanya, lakini kila kitu kinatokea kwasababu, so the time
is now naona, watu wakae tayari tu, chamsingi watu wakae tayari tu kwa
Hard Blasters". Jay
"kwa kiasi kubwa sana yupo kwenye kiwango
kizuri sana, kwasababu kuna wakati hali ilikuwa mbaya sana lakini Fanani
sasa hivi yupo fresh yupo free na tuko nae mda wote kwahiyo
tunajitahidi sana asirudi alipotoka, kwasabau ameamua kwa dhati.
unajua watu tunashindwa kuelewaga, mtu anapokuwa ameathirika na vitu
kama hivyo, pombe au madawa ya kulevya chakwanza kinachotakiwa ni yeye
mwenyewe kuacha kwa dhati, so tumehangaika nae kwa muda mrefu na sasa
hivi ameamua kuyaacha yale madude na hata kurudia kumeza matapishi yake,
kwahiyo tunatumaini tutafanikiwa......kwahiyo watu wategemee kumuona
clean the brand new Fanani, Faqnani mpya kabisa katika game. katika
akili na uwezo na hata kimuonekano yupo tofauti sasa hivi". amesema Jay
Social Plugin