Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BAD NEWS!! WANAFUNZI WA UHURU SEKONDARI WAFARIKI DUNIA WAKIOGELEA BWAWA LA NING'WA SHINYANGA



Habari zilizokifikia chumba cha habari cha Malunde1 blog ni kwamba wanafunzi wawili waliokuwa wanasoma katika shule ya sekondari Uhuru mjini Shinyanga wamefariki dunia wakati wakiogelea kwenye Bwawa la Ning'wa lililopo nje kidogo ya mji wa Shinyanga.

Kwa mujibu wa kaka wa mmoja wa wanafunzi hao Shabaan Alley ambaye ni mwandishi wa Star tv/Rfa aliyezungumza na malunde1 blog hivi punde kwa njia ya simu amesema mdogo wake na mwenzake  hawakuonekana nyumbani tangu jana jioni baada ya kutoka shuleni.

Amesema tangu jana jioni walikuwa hawajulikani walipo,na tangu jana walikuwa wanawatafuta  hadi walipogundulika jioni hii wakiwa wamefariki dunia katika bwawa la Ning'wa.


Habari zinasema wanafunzi hao Hussein Alley na Kaseja Stanley waliokuwa wanasoma kidato cha pili walikwenda kwenye bwawa hilo kuogelea na tangu jana walikuwa wanatafutwa.

Nguo zao na baiskeli waliyokuwa nayo vilionekana pembezoni mwa bwawa hilo ndipo wakagundulika kufa maji katika bwawa hilo leo jioni majira ya saa 11.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

BONYEZA MANENO HAYA UONE PICHA ZA MAZISHI

Malunde1 blog inawapa pole ndugu jamaa na marafiki wote waliofikwa na msiba.

Mungu azilaze mahali pema peponi roho za marehemu.Amina!!

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com