JK AWATOLEA UVIVU WAKUU WA WILAYA NA WAKUU WA MIKOA, HANA MZAHA NAO WATAOSHINDWA KUTIMIZA KUJENGA MAABARA ZA KIDATO CHA TANO NA SITA
Saturday, October 04, 2014
RAIS KIKWETE.
RAIS Jakaya Kikwete amesema atawajibisha wakurugenzi watakaoshindwa
kukamilisha ujenzi wa maabara ifikapo mwezi ujao kwani katika suala
hilo, hatakuwa na mzaha. Aidha amesema kuanzia sasa,
shule zote za sekondari za Serikali zenye Kidato cha Tano na Sita
zitakuwa za kitaifa, kwa maana ya kuwa na mchanganyiko wa wanafunzi
kutoka maeneo mbalimbali nchini, lengo likiwa ni kuendeleza utaifa kwa
vijana.
Rais Kikwete ambaye alisema hayo juzi mjini hapa wakati
akifungua kikao kazi cha kujadili usimamizi na uendeshaji wa Elimu ya
Msingi na Sekondari, aidha amewashukia wakuu wa mikoa na wilaya akisema
ambao hawajui wajibu wao ni bora wasiwepo.
Aliwaambia viongozi
hao wa wilaya na mikoa kwamba, “Kama ajenda yako ni barua na posho ni
bora usiwepo.’’ Wakurugenzi kitanzini Katika kikao hicho
kilichoshirikisha wakuu wa mikoa yote nchini, wakuu wa wilaya, maofisa
elimu wa mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na maofisa usalama, Kikwete
alisema wakurugenzi wakishindwa kuhakikisha kila shule inakuwa na
maabara, kazi itakuwa imewashinda.
Alisema alishatoa maagizo juu
ya ujenzi wa maabara za sayansi kwani mtoto anayesoma bila maabara,
hawezi kufaulu mtihani wa vitendo.
“Novemba nitauliza sina
sababu ya kusahau, nasubiri Desemba 9, mwaka huu wakati wa miaka 53 ya
uhuru nitauliza maswali na nitadai taarifa hizo lazima nizipate,”
alisema.
“Nitamuuliza Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na
Mkurugenzi, kama shule hazina maabara Mkurugenzi kazi imekushinda
nitaanza na wewe, Novemba mwaka huu tutabanana, bado nitakuwa na mamlaka
kamili na sitakuwa na masihara na mtu,” alisema.
Alisema katika
ujenzi huo anataka kuwa na maabara za fizikia, kemia na baolojia. “Kuna
mahali nilipita nikaoneshwa maabara nikanyamaza kimya nasubiri
Novemba,” alisema.
Alisema maendeleo yote ya nchi hii yapo mikononi mwa wakurugenzi.
“Lakini kama Mkurugenzi hatimizi wajibu wake kwa nini yupo na kwa nini anaendelea kuwepo?” alihoji.
Shule
za utaifa Akifafanua kuhusu utaifa kwa vijana, alisema kuanzia sasa
shule zote za serikali zenye kidato cha tano na sita zitakuwa za kitaifa
na hata zile ambazo ziko kwenye kata zitabadilishwa na lazima ziwe na
mabweni ya kulala wanafunzi.
“ Tunataka kuendeleza utaifa kwa
vijana, tuendelee kuwa na shule za taifa vinginevyo utakuta mtu
amezaliwa Kanyigo amesoma shule ya Msingi Kanyigo, Sekondari Kanyigo,
Kidato cha tano na sita Kanyigo mtu kama huyu anaelewa watu wote duniani
ni Wahaya,” alisema.
Aliendelea kusisitiza, “kidato cha tano na
sita lazima iwe ya taifa mwanafunzi akisoma Bukoba aende Ndanda
(Mtwara) hapo watajua kuchanganyika na vijana kutoka nchi nzima, wasome
shule hizo.”
Pia alisema sasa shule za kata zinaendelea
kutoshelezwa kwa ubora na wanafunzi wengi wanaochaguliwa kwenda kidato
cha tano na sita wanatoka shule za kata. Kuhusu uhaba wa walimu, alisema
serikali imepunguza tatizo katika shule za msingi na sekondari ambapo
mwaka jana walimu 18,000 waliajiriwa.
Alisema kwenye baadhi ya
wilaya, kuna ziada ya walimu wa sanaa lakini tatizo lililopo ni upungufu
wa walimu wa sayansi na hisabati, tatizo ambalo linaendelea kupatiwa
ufumbuzi. Mahitaji ni walimu wa sayansi na hisabati 18,277 huku uwezo
vyuo vyote ukiwa ni walimu 2,500.
Aliagiza mwaka 2016 kila mtoto
awe na kitabu chake cha kila somo. Wanafunzi Vyuo Vikuu Pia alisema
kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaoingia vyuo vikuu nchini
kutoka 40,000 mwaka 2005 hadi kufikia 204,000 na kuweza kufikia Wakenya
na kuwapita Waganda kwa idadi ya wanafunzi
Alisema Serikali
imetoa wigo mpana kwa vyuo vikuu na wanafunzi wote wanapata mikopo na
sasa hakuna mwanafunzi mwenye sifa anayeweza kukosa nafasi ya kujiunga
na Chuo Kikuu.
Alisema Chuo Kikuu cha Dodoma kilichojengwa kwa
fedha za ndani, kinachukua wanafunzi 20,000 na lengo ni kufikia
wanafunzi 40,000.
Alisema wanafunzi wataongezeka taratibu
kutokana na chuo hicho kuendelea kujitanua. Utoro Pia aliwataka viongozi
hao kuhakikisha watoto wanaoandikishwa shule ya msingi wanamaliza
Darasa la Saba tofauti na sasa ambapo wanafunzi wengi wamekuwa wakiacha
shule. Wakati huo huo, alitaka kulindwa kwa maeneo ya shule yasivamiwe
na wakurugenzi wasaidie vijiji kupata hati.
“Kila shule eneo lake linajulikana lipatiwe hati na liwekewe mipaka ili watu wasiliingilie,” alisema.
Pia
alitaka kuwe na matumizi mazuri ya fedha kwenye masuala ya elimu.
Viongozi waoga Alisema viongozi wengi ni waoga na si wabunifu hasa
katika suala la ujenzi wa nyumba za walimu.
Aliwataka
wakurugenzi kuacha kugeuza shule za sekondari yatima kwa kudhani wajibu
wao ni kusimamia shule za msingi tu. “Kila kata ina sekondari kabla ya
shule za kata zilikuwa chini ya wizara lakini sasa shule hizo ni za
halmashauri,” alisema.
Alitaka wakurugenzi kusimamia vizuri
walimu wapya waliopo katika maeneo yao wapate mishahara kama
wanavyostahili kwani kucheleweshewa fedha zao ni kutokana na uzembe
unaofanywa na baadhi ya watendaji Awali Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia alisema kikao
hicho cha siku tatu kinahudhuriwa na washiriki 908. Pia alisema kikao
hicho kimeridhia Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kuwa Chuo Kikuu Huria
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin