Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akiwa ndani ya Gari aina ya BMW 545i alilozawadiwa na meneja wake.
Achana
na lile gari aina ya Nissan Murano alilozawadiwa na mwandani wake,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, gari lingine aina ya BMW 545i
aliloletewa Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kwenye pati ya
‘bethidei’ yake ni utata mtupu na maswali kibao.
Pati
hiyo ambayo iliandika historia katika ulimwengu maridhawa wa mastaa
iliangushwa nyumbani kwa mwanadada huyo, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama
jijini Dar, wikiendi iliyopita ambapo alitimiza umri wa miaka 26.
Akiwa Marekani,
Diamond alimuagiza mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ apeleke gari aina
ya Nissan Morano lenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 36 za madafu
ikiwa ni zawadi ya jamaa huyo kwa mkewe huyo mtarajiwa.
Gari aina ya BMW 545i alilozawadiwa Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na meneja wake.
Alipoliona gari hilo, Wema alipigwa na butwaa huku akimshukuru Diamond ambaye kwa sasa amempachika jina la Chibu baada ya lile la Dangote ‘kueksipaya’.
MANENO KUNTU
Huku akiambatanisha
na picha ya gari hilo, kupitia ukurasa wake wa Instagram alimwandikia
Wema: “Nilitazama nikupe vingi huenda ingesaidia kukueleza ni kiasi gani
napenda nikuone ukiwa umefurahi kwenye siku yako hii ya
kuzaliwa...lakini tu sina uwezo huo Mumy...tafadhali pokea hicho kidogo
hiki nilichojaliwa leo.”
BMW UTATA MTUPU!
Gari aina ya BMW alilokabidhiwa na meneja wake, Martin Kadinda ndilo habari ya mjini huku nyuma yake kukiwa na maswali kibao.
Martin Kadinda akionyesha funguo ya Gari aina ya BMW aliyomzawadia Wema.
MAMA WEMA AHOJI
Wa kwanza kuhoji
alikuwa ni mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu ambaye alikataa kwamba
Kadinda hawezi kutoa zawadi ya gari kama hilo hivyo minong’ono ikawa ni
mingi.
Baada ya kuona hivyo,
Kadinda alitoa kadi ya gari hilo lenye namba spesho za usajili ambapo
jina la mmiliki lilisomeka Wema Sepetu.
MKONGO ATAJWA
Hata hivyo, pamoja na
utetezi wake, maneno yaliendelea kusambaa kama moto wa kifuu kwamba
nyuma ya gari kuna stori kubwa inakuja.
Muonekano wa keki ya ‘bethidei’ ya Wema.
Minong’ono mingine ilikwenda mbele zaidi huku jamaa mmoja mfanyabiashara kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Mkongomani) akitajwa kulinunua na kumpa Kadinda akakabidhi.
Baada ya kuona gari
hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 56 za madafu zinaleta utata,
kama kawaida yake, Kadinda alikimbilia kwenye ukurasa wake wa Instagram
akaandika:
“....Gari
hili linatokana na kazi ndogo tuzifanyazo na sapoti kubwa ya watu
wanaotutakia mema. Peke yangu nisingeweza bila sapoti yao....”
Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akimlisha keki mama yake.
MSISITIZO
Akizungumza na gazeti hili juu ya sakata hilo, Kadinda alisema kwa msisitizo: “Ni mimi ndiye nimemnunulia Wema hilo gari.”
MASWALI
Huku Kadinda
akisisitiza hivyo, waalikwa walibaki na maswali vichwani likiwemo lile
linaloulizwa zaidi kwamba iweje yeye (Kadinda) aendeleshe gari la
thamani ndogo aina ya Toyota Corola halafu ampe Wema BMW?
“Hapa pana kitu na
kitakapobumburuka itakuwa soo, ni bora Kadinda angefunguka ukweli kuliko
kuja kunyooshewa vidole baadaye, ngoja tusubiri,” alisikika mmoja wa
mastaa walioalikwa (jina kapuni).
Akimlisha keki mamamkwe wake.
MENGINE YATOKANAYO
Pati hiyo ya Wema iligawanyika mara mbili ambapo ya kwanza ilianza saa 6:00 mchana hadi saa 12:00 huku nyingine iliyohusisha watu maarufu ikianza baadaye hadi ‘kokoriko’.
KEKI 69 MEZANI
Katika hali isiyo ya
kawaida, sherehe hiyo ilikuwa na keki zipatazo 69 ambazo zililetwa na
baadhi ya mastaa ambao walihudhuria sherehe hiyo huku kukiwa na vinywaji vya kufa mtu (wiski tu), loko bia tupa kule.
Akimlisha keki Jokate.
NDAFU
Kwa upande wa nyama kulikuwa ndafu mzima ambaye watu walimtafuta hadi wakasaza.
MAMA DIAMOND AMTANGAZA RASMI MKWEWE
Katika sherehe hiyo,
mama Diamond alipopewa kipaza sauti ‘maiki’ ili anene chochote alisema
kuwa Wema ni mkwe wake wa halali na kwamba anampenda hivyo asiwe na
wasiwasi kwani hakuna mkwe mwingine atayatokea zaidi yake.
Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akifungua shampeni kwaajili ya shughuli hiyo.
“Jamani huyu ndiye mkwe wangu, Mrs Chibu (Diamond) ndiye mkwe wangu hasaaa...,” alisema mama Chibu huku watu wakishangilia.
MILIONI 10
Kwa mujibu wa Kadinda,
shughuli hiyo iligharimu zaidi ya Sh. milioni 10 hadi kukamilika na
kuonekana ya tofauti na pati nyingine za mastaa Bongo.
Wema akiongea jambo kabla ya kukata Ndafu.
AMWAGIWA NOTI
Ulipofika muda wa kutunzwa zawadi, watu walijitokeza kumtunza Wema fedha ambazo hazikuweza kupatikana kiasi chake mara moja huku staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiweka rekodi kwa kumwaga ‘minoti’ mingi katika hafla hiyo.
Social Plugin