Habari zilizotufikia kutoka mkoani Tabora ni kwamba basi la NBS lililokuwa linatoka jijini ,Mwanza kwenda Mpanda,limegonga punda leo asubuhi na kupinduka katika eneo la Nzega Ndogo.
Punda aliyesababisha ajali hiyo leo akiwa amekufa
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia ni kwamba mtu mmoja,ambaye ni kondakta wa basi hilo amefariki dunia na majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Nzega.Inaelezwa kuwa majeruhi 12 wako mahututi
Social Plugin