Habari za hivi punde zilizoufikia mtandao huu wa malunde1 blog ni kwamba rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) na mwenyikiti wa baraza la mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein leo amemfuta kazi mwanasheria mkuu wa Zanzibar Othman Masoud Othman na nafasi yake kuchukuliwa na Said Hassan Said. Rais Shein amefanya uteuzi huo wa mwanasheria mkuu wa serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 55(1) cha katiba ya Zanzibar 1984. Said Hassan Said ameteuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar ambapo uteuzi huo umeanza leo Oktoba 7,2014. Kabla ya uteuzi huo alikuwa naibu mwanasheria mkuu. Uteuzi wa Othman Masoud Othman umefutwa kwa mujibu wa vifungu vya 53,54(1) na 55(3) vya katiba ya Zanzibar ya 1984 na kifungu12(3) cha sheria ya utumishi wa umma namba 2 ya mwaka 2011. |
Social Plugin