Habari Zilizotufikia hivi punde zinaeleza kutokea kwa ajali ya bus la Simba mtoto na lori zimegongana uso kwa uso eneo la Wami ila taarifa za awali zimebainisha kuwa dereva wa lori amefariki papo hapo huku abiria wa simba mtoto baadhi yao kupatwa na majeruhi.
Ajali mbaya hiyo imetokea leo eneo la daraja la Wami baada break za Lori kufeli na kugongana na basi hilo.Dereva wa Lori amepoteza maisha hapohapo.
Basi la Simba mtoto linalofanya safari zake kati ya Dar na Tanga likiwa limegongana uso kwa uso na Lori la mizigo katikati ya Daraja la Mto Wami mkoani Pwani,dereva wa lori hilo amefariki papo hapo na wengine kujeruhiwa.tutaendelea kupeana taarifa zaidi hapo baadae.
Social Plugin