HILI ni fumanizi la aina yake! Achana na mafumanizi ya kawaida ambayo yamezoeleka, la safari hii ni la kipekee baada ya mgoni aitwaye Kibole Kalepe kukutwa chumbani na mke wa mtu, Asha Hemedi kisha kukurupuka na kupanda darini haraka kukwepa kipigo.
Tukio hilo lililofunga umati wa watu wapenda ubuyu lilijiri Oktoba 28, mwaka huu maeneo ya Iteba-Sinza, jijini Dar baada ya mwenye mali, aitwaye Fikiri kurejea ghafla nyumbani na kumkuta mkewe akiwa chumbani na Kibole wakifanya yao.
Mke wa mtu, Asha Hemedi akihamaki baada ya fumanizi.
SIKU YA TUKIO
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio Fikiri ambaye ni dereva wa masafa marefu aliaga kwamba anasafiri lakini akiwa hajafika mbali, gari liliharibika na kurudi nyumbani kuchukua vifaa na kabla hajagonga mlango, alisikia sauti ya mkewe na Kibole.
UVUMILIVU WAMSHINDA
Chanzo hicho kilizidi kushusha mistari kwamba, baada ya kusikia sauti hizo, Fikiri hakuweza kuvumilia aliamua kuwakatisha kwa kuwagongea mlango huku akitaja jina la mkewe ili amfungulie lakini hata hivyo ilichukua muda mrefu mlango kufunguliwa.
MLANGO WAFUNGULIWA
“Mume aliendelea kugonga mlango, baada ya muda mrefu kupita ukafunguliwa ambapo mke alikutwa akiwa ameloa jasho na kuhema kwa kasi kutokana na hofu, hata hivyo alikua amefunga khanga moja tu.
MGONI JUU YA DARI
“Mume alipoangalia kila kona kumtafuta mwanaume aliyekua naye hakumuona na alipochungulia darini alimuona mgoni wake amejificha, baadaye aliomba wapigiwe simu polisi waje kumuokoa,” kilisema chanzo.
ACHIMBWA MKWARA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kwamba, wananchi wapenda mambo ya watu waliokuwa wamezingira nyumba hiyo walimwambia yeye ni mwizi hivyo watamshushia kipondo hevi, mgoni huyo alikataa na kudai kwamba hakuwa mwizi bali mgoni hivyo wasimuue.
“Jamani mimi siyo mwizi mimi ni mgoni, niitieni polisi,” alisikika Kibole.
POLISI WAMTAITI
Wananchi walimuelewa wakaita polisi ambapo ndani ya muda mfupi walifika na kumshusha darini kisha kumkamata na mwananke wakawapeleka Kituo cha Polisi Magomeni.
MAKONGORO OGING’ NA HARUNI SANCHAWA
Social Plugin