HAYA NDIYO MATUKIO YA MWENGE WA UHURU WILAYA YA SHINYANGA,TAZAMA PICHA HAPA
Sunday, October 05, 2014
HALMSHAURI YA SHINYANGA Oktoba 4,2014-Hapa ni katika kijiji cha Mwakitolyo.Pichani ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi akimkaribisha/akishikana mkono na kiongozi wa mbio za mwenge 2014 Rachel Stephen Kassanda (kushoto) baada ya mwenge huo kuwasili katika wilaya ya Shinyanga ukitokea wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga-Picha na Kadama Malunde
Mradi wa maji wa maji kijiji cha Mwakitolyo ambapo kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru aliweka jiwe la msingi-Picha na Kadama Malunde
Hapa ni katika shule ya msingi Ng'wakitolyo iliyoanzishwa mwaka 1964.Pichani ni kiongozi wa mbio za mwenge Rachel Kassanda akizungumza na wananchi wa Mwakitolyo ambapo aliwataka kuachana na imani za kishirikina ili kuepukana na mauaji ya vikongwe kwani mauaji hayo yanatokana na watu kutomjua mungu na kuendekeza waganga wa kienyeji wenye ramla chonganishi-Picha na Kadama Malunde
Hapa ni katika kijiji cha Lyabukande,kushoto ni mkimbiza mwenge wa uhuru 2014,Luteni Tanu Oscar Mlowezi akikabidhi hundi ya shilingi laki 3 kwa kundi la wanawake katika kijiji cha Lyabukande na Mwamagunguli,lakini pia alitoa hundi ya shilingi milioni 3 kwa kundi la vijana katika eneo hilo-Picha na Kadama Malunde
Hapa ni katika soko la kisasa katika kijiji cha Didia kata ya Didia ambapo kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu aliweka jiwe la msingi-Picha na Kadama Malunde
Mkimbiza mwenge wa uhuru 2014 Wito Mlemelwa akikagua soko la kisasa la Didia kwa niaba ya kiongozi wa mbio za mwenge taifa Rachel Kassanda-Picha na Kadama Malunde
Mkimbiza mwenge wa uhuru 2014 Wito Mlemelwa akitoa ujumbe wa mwenge mwaka huu,katika shule ya msingi Didia ambapo alisisitiza umuhimu wa kuenzi mwenge wa uhuru na kuwa wazalendo pamoja na kupiga vita rushwa kuanzia mashuleni kwani watoto wanaanza /dalili za ufisadi wakiwa wadogo mfano kiranja na monita wa darasa-Picha na Kadama Malunde
Hapa ni katika shule ya sekondari ya wasichana Tinde,ambapo kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu alifungua maabara na kuona shughuli za klabu ya wapinga rushwa na kukabidhi cheti kwa shule hiyo-Picha na Kadama Malunde
Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu Rachel Kassanda akiangalia shughuli zinazofanywa na klabu ya wapinga rushwa katika uwanja wa Tinde shule ya msingi,ambapo katika mbio hizo za mwenge katika halmashauri ya Shinyanga mbunge wa viti maalum Azzah Hilal alikuwepo(yupo nyuma ya Rachel Kassanda)-Picha na Kadama Malunde
MANISPAA YA SHINYANGA 0ctoba 5,2014-Hapa mi katika Chuo cha Ufundi stadi VETA mjini Shinyanga,kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru na msafara wake na wakiangalia shughuli zinazofanywa na wanafunzi katika chuo hicho.Pichani greda linaloendeshwa na mwanafunzi wa kike likitengeneza barabara-Picha na Kadama Malunde
Mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi akiwasalimia wanafunzi wa chuo cha VETA na wananchi waliofika chuoni hapo kuangalia mwenge ambapo alitumia maneno kutoka mwenye biblia kuwatahadhalisha watanzania kulinda amani ya nchi na kuwataka wafanye kazi huku akiwaasa wanafunzi kutumia chuo cha VETA kusoma kwa bidii-Picha na Kadama Malunde
Kushoto ni kiongozi wa mbio za mwenge Rachel Kassanda,akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Anna rose Nyamubi na mbunge wa jimbo la Shinyanga mjin Stephen Masele/naibu waziri wa madini nchini wakifuatilia,wakifurahia hotuba fupi ya mheshimiwa Suleiman Nchambi mbunge wa Kishapu ambaye aliamua kuungana na wakazi wa manispaa ya Shinyanga kukimbiza mwenge wa uhuru na kesho Octoba 6,2014 mwange huo utakuwa wilayani Kishapu-Picha na Kadama Malunde
Watoto wakiwa katika chuo cha VETA kuona mwenge wa Uhuru-Picha na Kadama Malunde
Watoto wenye ulemavu wa ngozi kutoka katika shule ya msingi Buhangija jumuishi wakishika mwenge wa uhuru katika shule ya msingi Little Treasures mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde
Ni katika shule ya msingi Little Treasures mjini Shinyanga ambako kiongozia mbio za mwenge mwaka huu aliweka jiwe la msingi na kuona mradi wa mazingira(jiko la kisasa)-Picha na Kadama Malunde
Ni katika shule ya msingi Little Treasures mjini Shinyanga kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu Rachel Kassanda akiweka chambo kwenye mizinga ya nyuki-Picha na Kadama Malunde
Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu Rachel Kassanda akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wanofundishwa kwa lugha ya kiingereza pekee,shule ambayo iko mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde
Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu Rachel Kassanda akimtwisha ndoo ya maji Agnes Maganga katika kijiji cha Mwamagunguli katika kata ya Kolandoto baada ya kufungua mradi wa maji/kufungua tanki la maji-Picha na Kadama Malunde
Hapa ni katika kijiji cha Mwamagunguli katika kata ya Kolandoto eneo la mradi wa maji ya ziwa Victoria,mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele akiwasalimia wananchi wa Kolandoto-Picha na Kadama Malunde Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu Rachel Kassanda akizungumza na wananchi wa Ibadakuli baada ya kuona vikundi vya akina mama wafinyanzi wa vyungu katika kata hiyo ambapo alisisitiza umuhimu wa wanawake kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ili wajikwamue kiuchumi badala ya kutegeme wanaume kila kukicha-Picha na Kadama Malunde
Kazi ya akina mama wafinyanzi wa vyungu,wanatengeneza hadi vyungu vyenye umbo la Sufuria-Picha na Kadama Malunde
Kiongozi wa mwenge kitaifa Rachel akiwa katika eneo la mnada wa Old Shinyanga ili kuweka jiwe la msingi uzio wa mnada
Mradi wa Mobile Cuts Vending Chips kutoka shirika la Agape,mradi unafanyika kwa kutembeza chips mtaani kupitia usafiri huo pichani-Picha na Kadama Malunde
TAREHE 6-10-2014 MWENGE WA UHURU UTAKIMBIZWA KATIKA WILAYA YA KISHAPU NA TAREHE 7,10,2014 UTAKABIDHIWA MKOA WA TABORA UKITOKEA MKOA WA SHINYANGA
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin