Richard Mileski, mmiliki wa hifadhi aliyeuawa na ngamia.
Richard Mileski (60), aliyekuwa mmiliki wa hifadhi ya wanyama pori nchini Mexico ameuawa kikatili na ngamia aliyekuwa akimfuga katika hifadhi hiyo kutokana na kutompatia ngamia huyo ‘dozi’ ya soda aliyomzoesha kumpatia.
Taarifa kutoka mtandao wa rt.com zinasema ngamia huyo alimvamia Mileski ndani ya hifadhi hiyo na kumpiga mpaka kuishiwa nguvu, na baada ya kuanguka chini ngamia huyo alimkalia juu yake kitendo kilichopelekea mtu huyo kufariki.
Maafisa usalama waliofika katika eneo hilo, walilazimika kumfunga kamba ngamia huyo na kumvuta kwa gari ndogo ili waweze kuutoa mwili wa marehemu huyo.
Taarifa za awali zinasema huenda ngamia huyo alikasirishwa na kitendo cha Mileski kutompatia soda aina ya Coca cola alichozoea kumpatia.
Mileski alianzisha hifadhi hiyo maalum aliyoipa jina la ‘Tulum Monkey Sanctuary’ kwa ajili ya kuhifadhi nyani na buibui ambao walikuwa wakitoweka nchini humo, na baadaye aliongeza wanyama wengine, japo serikali imesema alianzisha hifadhi hiyo bila ya kuwa kibali wala leseni.
Kwa miaka 15 Mileski amejitolea maisha yake kwa kuhifadhi wanyama katika hifadhi hiyo iliyojizolea umaarufu kwa shughuli za utalii.
Mtandao wa China.org.cn wa China umemtaja ngamia huyu ni mnyama wa kwanza kufanya mauaji ya kikatili zaidi duniani.
Social Plugin