Kilabu
ya watoto walio kati ya umri wa miaka 6 na 12 ilifunguliwa rasmi katika
mji wa New York wilaya ya meatpacking nchini Marekani.
Mgahawa
huo unaomilikiwa na kampuni ya Cirkiz utakuwa ukifunguliwa mara moja
kila mwezi kuwapa watoto fursa ya kujivinjari mbali na vifaa vya
kiteknolojia vilivyomo majumbani mwao.
Laura lampart aliyekuwa
ameandamana na mwanawe alisema kuwa kilabu hiyo ina manufaa kwani watoto
walijihisi kama watu wazima na hakukuwa na tatizo la kuhofia usalama
kwani Mgahawa wenyewe unafunguliwa wakati wa mchana.
Kati ya vinavyojumuishwa ni wanadensi ambao ni watoto wanaowatumbuiza wenzao na pia ma Dijei ambao pia ni watoto.
Zaidi ya watu 300 wakiwemo wazazi na watoto walihudhuria ufunguzi huo.
Mtindo huo umepata umaarufu katika miji miingine kama vile South Korea,Berlin na Los Angeles.
via>>BBC