BAADA ya kuvuja kwa picha katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita, iliyowaonesha askari wawili wa usalama barabarani wakiwa ‘kimahaba niue’ ndani ya sare za kazi na kusababisha kupoteza ajira zao kutokana na kukiuka maadili, siri zaidi nzito zimezidi kuvuja kuhusiana na ishu hiyo sasa ameibuliwa afande wa kike baada ya kumsaka sana.
Kwa mujibu wa vyanzo makini kutoka wilayani Misenyi mkoani Kagera, askari wa kike aliyeonekana kwenye picha hiyo chafu, WP. 8898 Veronica Mdeme, inadaiwa kuwa alipata uhamisho kutoka polisi mkoani humo na kupelekwa katika wilaya mpya ya Misenyi mwaka 2011 ambako mwaka mmoja baadaye, ndipo akapigwa picha hiyo iliyoleta gumzo kubwa ndani na nje ya Bongo.
Ilidaiwa kwamba, picha hiyo ilipigwa katika barabara ya lami iendayo Mutukura, umbali wa Kilomita 50 kutoka Misenyi na kwamba askari hao walikuwa katika Kituo cha Polisi cha Kyaka.
Nguzo ya umeme inayoonekana nyuma yao, ni zile zinazopeleka umeme nchini Uganda kutoka Bwawa la Umeme la Mtera, Tanzania.
ILIKUWA PICHA YA KISHKAJI TU LAKINI…
Habari zilidai kuwa, askari hao Veronica, F.7788 Mpaji Mwasumbi na PC Fadhil Linga, walikuwa zamu moja na kwamba picha hiyo ilipigwa katika mazingira ya kishkaji tu lakini baadaye ikaja kuzua balaa kubwa.
Ilisemekana kwamba, Linga ndiye aliyewapiga picha wenzake ambao habari zisizothibitishwa zilisema kuwa walikuwa na uhusiano wa kijamii.
Madai yalizidi kutiririshwa kwamba baada ya kupigwa kwa picha hiyo, Linga alibaki na nakala katika kamera yake kwa muda wa miezi kadhaa kabla ya kugundua kuwa kumbe ilikuwa ni dili.
AWAGEUZIA KIBAO
Ilidaiwa kwamba, katika hali isiyotarajiwa, Mpaji na Veronica hawakuamini masikio yao baada ya Linga kuwaambia kwamba alihitaji kupata ‘kitu kidogo’ kutoka kwao ili aweze kuendelea kuhifadhi siri ya picha hizo.
Ilisemekana kuwa afande huyo aliwaambia wawili hao kama ataivujisha picha hiyo kwenye mitandao ya kijamii, watapoteza kazi.
kilidai chanzo hicho.
WAAMUA KUJILIPUA, WAMSHTAKI
Ilielezwa kwamba, baada ya ‘kutolewa upepo’ kwa muda mrefu na kuonekana kama wangekuwa ATM ya kudumu ya Linga, Mpaji na Veronica waliamua kujilipua na kwenda kumshtaki kwa kigogo wa juu wa jeshi la polisi mkoani humo ambaye anatajwa kuujua mchezo mzima ulivyokuwa.
Ilisemekana kwamba, kiongozi huyo alilichukulia jambo hilo kwa uzito wake na kuwakalisha wote watatu ili kuzungumza nao.Iliendelea kudaiwa kuwa katika kikao kati ya askari hao na bosi wao, wawili hao walikiri kupigwa picha hiyo na kuomba msamaha, lakini wakamlalamikia mwenzao ambaye naye alikiri kufanya kitendo hicho, kwa kuwageuza kuwa ATM.
Ilidaiwa kuwa mkubwa huyo alimuamuru Linga kuzifuta picha hizo na kuwataka kusameheana, kwani kitendo walichokifanya ni kibaya na kinachoweza kuhatarisha ajira zao. Linga alikubali ‘kuzi-diliti’ picha hizo!
WAGAWANYWA, LINGA ARUDIA
Ikazidi kudaiwa kuwa ili kuwafanya waishi kwa amani, waligawanywa katika vituo tofauti vya kazi mkoani humo huku mmoja wao, Mpaji akipelekwa Dar ambako alikwenda kusoma Chuo cha Polisi Kurasini.
kilisema chanzo chetu.
Inaelezwa kwamba majibu ya jeuri kutoka kwa Vero na Mpaji yalimuudhi Linga ambaye kwa lengo la kuwakomoa, aliamua kuzitupa picha hizo katika mitandao mbalimbali ya kijamii ambako nako zilizagaa kwa kasi ya moto wa kifuu na kuwafikia watu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari vilivyoamua kuripoti.
kilisema chanzo hicho.
PICHA YA MREMBO YAWA GUMZO
Baada ya kufukuzwa kazi kwa wahusika hao watatu, kumekuwa na picha za mrembo mkali ambaye amekuwa akifananishwa na Veronica huku kukiwa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kama kweli ni yeye (angalia picha hapo juu).
Kwa mujibu wa maoni lukuki katika mitandaoni, kama kweli mrembo huyo ndiye huyo askari wa kike, basi jamaa aliyekuwa naye kimahaba, alistahili adhabu yoyote kuliko kukosa mahaba hayo.
ilisomeka sehemu ya maoni ya stori hiyo ambayo ndiyo habari ya mjini kwa sasa.
Juzi, meza yetu ya habari imemtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe ili kumsikia nini kinaendelea baada ya askari hao kufukuzwa kazi lakini hakuwa hewani.
Naye msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Advera Senzo alipopigiwa simu na kuulizwa alisema walishafukuzwa kazi hakuna kingine lakini akaelekeza apigiwe simu Mwaibambe.
Social Plugin