Kama kila siku huwa unaingia facebook, whatsapp au instagram inawezekana ukawa ulikutana na hii picha ya Askari Polisi ambao walipigwa picha wakiwa wanakiss wakiwa ndani ya sare za jeshi hilo.
Sasa taarifa mpya iliyotoka baada ya hii picha kuzidi kusambaa ni kwamba Jeshi la Polisi Kagera limechukua maamuzi ya kuwafukuza kazi askari hawa wawili pamoja na mwingine mmoja ambae ndio aliipiga hii picha kupitia simu yake ya mkononi.
Soma habari kamili hapa
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani waliopiga picha ya mahaba wakibusiana huku wakiwa wamevaa sare za Jeshi la Polisi na picha yao ikasambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii wamefukuzwa kazi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe amethibitisha leo kwa waandishi wa habari mkoani humo kuwa, askari hao na mwenzao aliyewapiga picha wametambuliwa na tayari wamefukuzwa kazi kwa kitendo hicho cha kulidhalilisha Jeshi la Polisi.
Kamanda Mwaibambe amewataja askari hao kuwa ni PC Asuma Mpaji Mwasumbi mwenye namba F.7788, PC Fadhiri Linga mwenye namba G 2122 na PC Veronica Nazaremo Mdeme, wote walikuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Misenyi, mkoani Kagera.
Alisema kuwa PC Fadhiri ndiye aliyehusika na kupiga picha hizo kwa kutumia simu yake ya kiganjani na kuituma katka mitandao mbalimbali ya kijamii kitendo ambacho ni kinyume cha maadili kwa sababu mbalimbali. Amezitaja sababu hizo kuwa ni kupiga picha wakati wakijua kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha maadili ya jeshi hilo pamoja na kuituma picha hiyo kwenye mitandao mbalimbali. Aidha, Mwaibambe amekiri kuwa picha husika inayoonekana kwenye mitandao ni picha halisi ambayo haijachakachuliwa, hivyo ni wazi kila askari kujua kuwa maadili ya kijeshi yapo kisheria na askari yeyote anafundishwa namna ya kuishi katika maisha ya utumishi wa jeshi la Polisi. |
Social Plugin