Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha |
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia mganga
wa kienyeji bwana Mtabanzila Buyiyi(70)mkazi wa mtaa na kata ya Malunga
wilayani Kahama kwa kosa la kukamatwa akiwa na bunduki mbili aina ya gobore
zisizokuwa na namba zikiwa na hirizi akimiziliki kinyume cha sheria.
Malunde1 blog inaarifiwa kuwa tukio hilo
limetokea juzi saa tano na dakika 41 asubuhi wakati askari polisi
wakiwa doria na msako katika kata ya Malunga wilayani Kahama na kufanikiwa kukamata bunduki mbili aina ya gobore zisizokuwa na namba zikiwa zimefungwa hirizi na vipande vya ngozi ya mnyama asiyefahamika katika nyumba ya mganga huyo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha amesema bunduki hizo zilikuwa zinamilikiwa kinyume cha sheria na
zinadaiwa kutumika kufanya matukio ya uhalifu sehemu mbalimbali za mkoa
wa Shinyanga.
Aidha amesema pia wanamshikilia mtoto wa mganga huyo bi Nyamisi Mtabanzila(40) kwa kosa la kuendesha shughuli za uganga na baba yake bila leseni.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
Social Plugin