Katibu
mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Mazingira Tanzania (JET) John
Chikomo, akitoa taarifa yake ya utendaji pamoja na fedha mbele ya
mkutano mkuu wa mwaka 2013 wa chama hicho. Mkutano huo uliohudhuriwa na
wananchama wengi, ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Lion
iliyopo Sinza jijini Dar-es-salaam.Wa pili kushoto (waliokaa) ni
mwenyekiti wa JET, Johnson Mbwambo na anayefuata ni katibu christom
Rweyemamu na wa kwanza kulia ni mjumbe wa kamati ya bodi.
Na Nathaniel Limu, Dar es Salaam
MWENYEKITI
wa Chama cha waandishi wa habari mazingira Tanzania (JET),Johnson
Mbwambo,amewahimiza wanachama kuongeza juhudi kuandika habari na makala
zinazohusu mazingira, ili pamoja na mambo mengine, nchi yetu iwe mahali
salama pa kuishi.
Mbwambo
aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akifungua mkutano mkuu wa JET
wa mwaka 2013,uliofanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Lion iliyopo Sinza
jijini Dar-es-salaam.
Alisema uharibifu wa mazingira ni mkubwa mno hivi sasa,na pamoja na madhara yake mengi,pia unatishia nchi kugeuka kuwa jangwa.
Mbwambo
alisema kuiepusha nchi kugeuka jangwa,kila mwanachama wa JET anao
wajibu wa kuandika habari na makala nyingi zinazoelimisha jamii juu ya
madhara ya uharibifu wa mazingira.
Baadhi
ya wanachama wa JET kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini waliohudhuria
mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyikia kwenye ukumbi wa mikutano wa
hoteli ya Lion iliyopo Sinza jijini Dar-es-salaam.(Picha na Nathaniel
Limu).
“Nasikitika
kusema kwamba wanachama wengi hawaitendei haki JET. Hawaandiki habari
wala makala zinazohusu uboreshaji wa mazingira, utunzaji wake na madhara
yatokanayo na uharibifu wa mazingira.Wengi ni wanachama wa JET kwa
ajili ya kuhudhuria tu mkutano mkuu”,alifafanua mwenyekiti huyo ambaye
ametamka wazi kuwa mwakani,hatagombea nafasi hiyo.
Kwa
upande wake katibu wa JET, Christom Rweyemamu alisema wanachama wengi
wanalipa ada zao kwa shida sana, hata wanapokumbushwa,hawalipi kama
inavyotakiwa.
“Aidha,wafadhili
wa kugharamia shughuli zetu nao wanaendelea kupungua.Kwa hiyo kuna haja
kubwa kujiangalia upya huko tuendako”,alisema.
Kwa
mujibu wa katibu mtendaji mkuu wa JET,John Chikomo, katika mwaka wa
fedha wa 2014, JET inatarajia kukusanya mapato ya zaidi ya shiligi 219.7
milioni kutoka mapato yake mbalimbali ikiwemo ada ya wanachama.Matumizi
yanatarajiwa kuwa shilingi 215,899,800.
Social Plugin