Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha
Mwanamme mmoja aliyejulikana kwa jina moja la
Sabo mwenye umri wa miaka kati ya 30 hadi 34 ameuawa kwa kupigwa mawe na fimbo na wananchi waliojichukulia sheria
mkononi kisha mwili wake kuchomwa moto baada ya kutuhumiwa kuiba ng’ombe wawili
katika kijiji cha Shininga kata ya Kilago,tarafa ya Dakama wilaya ya Kahama
mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP
Justus Kamugisha tukio hilo limetokea jana saa 11 jioni ambapo mwanamme huyo
mkazi wa Chibiso alipigwa na wananchi hao baada ya kumtuhumu kaiba ng’ombe
wawili mali ya mtu ambaye hakufahamika jina wala makazi yake na thamani ya ng’ombe
hao haijulikani.
Kamanda Kamugisha amesema chanzo cha tukio hilo ni
wananchi kujichukulia sheria mkononi na kwamba jeshi la polisi linaendelea na
msako kuwabaini na kuwakamata wahusika wote wa mauaji hayo.
Hata hivyo ametoa wito kwa
wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wahusika wa mauaji ha
yo
huku akiwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwa
kisingizio cha hasira kali kwani kitendo hicho ni ukiukwaji wa sheria za nchi
na haki za binadamu.
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Social Plugin