Dereva wa
gari la mwenyekiti wa baraza la wanawake Chadema taifa ambaye ni mbunge wa Kawe Halima Mdee
amekamatwa na kushikiliwa na jeshi la polisi kwa muda wa saa moja kisha
kumuachia wilayani Geita mkoani Geita .
Tukio hilo
limetokea leo asubuhi majira ya saa 3
mara baada ya dEreva huyo Joseph James anayeendesha gari lenye namba T374
BKE alipokuwa anatoa gari kwenye hotel ya Alfa walipofikia ili aende kuifanyia
matengenezo madogo mamadogo kabla ya kuelekea Busanda kwenye mkutano.
Mwandishi wa Malunde1 blog Valence Robert anaripoti kuwa dereva huyo baada ya
kutoka alikuta polisi wapo nje na walipomuona walimwamuru waende naye polisi kutokana na kile kilichodaiwa kuwa gari hilo lilitumika jana kukamata watuhumiwa
waliokuwa kwenye mkutano wa hadhara mjini Geita waliokuwa wanarekodi kilichokuwa kinajiri katika mkutano huo na kuwanyang’anya kinasa sauti(tape recorder)
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumtoa dereva polisi,Naibu katibu
mkuu wa Bawacha taifa Kunti Yusuph amesema jana wakati
wanafanya mkutano katika Viwanja vya Stand ya zamani mjini Geita watu wawili waliokuwepo mkutano walikamatwa na Red Brigade baada ya kuwabaini kuwa
wanarekodi mkutano kisiri.
Amesema mbali na kurekodi kilichokuwa kinaendelea pia wengine walijifanya kuwa ni wananchama wa Chadema.
Aliongeza
kuwa baada ya kuwashtukia watu hao ambao mmoja ni wa kike na mwingine wa kiume waliwakamata na kuwapeleka kituo cha polisi wakiwa na tape recoder mbili pamoja
na simu mbili.
Anasema walipowafikisha polisi walirudi mkutanoni na kwamba watarudi polisi baada ya kumaliza mkutano.
Baada ya
kwenda polisi walikuta watuhumiwa wao wameachiwa.
Mmoja wa watu hao alikuwa na kadi ya Chadema yenye namba 2155260
iliyotolewa tarehe 3.10.2014 kwa jina la Erenest J.Silayo anayedaiwa kuwa ni
askari polisi.
Mkuu wa
polisi wilayani Geita Silvester Ibrahimu alipoulizwa juu ya suala hilo alisema
kuwa dreva huyo alikamatwa na kukamatwa ni jambo la kwaida lakini hakueleza sababu ya kukamatwa kwake.
Hata hivyo alikiri kuwa wale
walikuwa watu wao waliwatuma kufanya kazi.
Na Valence Robert-Malunde1 blog Geita
Social Plugin