Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete na rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dk Ally Mohamed Shein wamekabidhiwa katiba iliyopendekezwa na bunge maalum la katiba ikiwa ni hatua muhimu katika historia ya Tanzania kuelekea kupata katiba mpya ambayo kwa mara ya kwanza imehusisha maoni ya wananchi, makundi maalum, taasisi wanasiasa na viongozi mbalimbali tangu taifa kupata uhuru wake.
Majira ya saa sita na nusu mchana ndipo makundi mbalimbali ya wageni waalikwa, viongozi wa juu wa serikali mabalozi marais na mawaziri wa kuu wastaafu wakaingia katika viwanja vya jamuhuri na kisha majira ya saa tisa na nusu rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dk Ally Mohamed Shein akawasili na kufuatiwa na rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Mara baada ya itifaki ya uongozi kuwasili shughuli ikaanza rasmi ambapo mwenyekiti wa kamati ya uandishi ya bunge maalum Mhe Adrew Chenge akaelezea maudhui ya katiba iliyopendekezwa pamoja na mambo mengine akasema katiba hiyo ina jumla ya sura 19 na ibara 296 na nyongeza tatu ambapo rasimu ya awali iliyowasilishwa bungeni ilikuwa na sura 17 na ibara 211 huku suala la muundo wa serikali likisalia kuwa serikali mbili.Nao wawakilishi wa makundi 15 ya kijamii yalisyoshiriki katika bunge hilo maalum la katiba walipata fursa ya kuelezea namna walivyowakilisha na kile walichokubaliana kiwepo katika katiba mpya.
Na kisha kile ambacho kilikuwa kikisubiriwa katika hastoria ya taifa kikawadia ambapo aliyekuwa mwenyekiti wa bunge maalum akakabidhi rasimu ya katiba iliyopendekezwa kwa rais wa jamuhuri Dk Jakaya Kikwete na rais wa Zanzibar Dk Ally Muhamad Shein.
Baada ya makabidhiano hayo viongozi hao wakuu wa taifa kuhusu mchakato wa katiba ambapo wameelezea matumaini yao makubwa kuhusu katiba hiyo pendekezwa.
Nao baadhi ya wanachi waliohudhuria siku hii hadhimu kwa mustakabali wa taifa walikuwa walitoa maoni yao kuhusu mchakato mzima wa uundwaji wa katiba mpya huku wakiwataka watanzania kuwa watulivu katika kipindi chote na watumie vizuri kura ya maoni ili kupata katiba itakayokuwa mwarubaini wa kutatua changamoto zinazolikabili taifa na yenye mlengo wa kimaendeleo.
Social Plugin