Viongozi
wa juu wa vyama vinne vya siasa nchini Tanzania vimeingia makubaliano ya
ushirikiano wa shughuli mbalimbali za siasa hii leo na miongoni mwa
mambo hayo ni kusimamisha wagombea wa pamoja katika uchaguzi wa Serikali
za Mtaa na Uchaguzi Mkuu wa wabunge, madiwani, wawakilishi na Rais
2015. Kutoka kushoto ni James Mbatia wa NCCR-MAGEUZI, Prof Ibrahim
Li[pumba wa chama cha Wananchi CUF, Freeman Mbowe wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Dk. Emmanuel makaidi wa NLD
wakionesha hati yao ya makubaliano waliyoisaini katika viwanja vya
Jangwani Dar es Salaam
Wafuasi,
wanachama, wa vyama vya siasa vinavyounda ukawa wakifuatilia mkutano huo
ambao ulianza kwa kuimba wimbo wa Taifa huku wanachama hao wakiwa
wamekaa jambo ambalo lilielezwa na viongozi wao kuwa uzalendo ni ndani
ya moyo. Chini ndio mambo waliyokubaliana.
Social Plugin