Kijana wa miaka kumi na 19 anayeitwa Jamal Nasiru kutoka Nigeria amekamatwa na chombo cha dola kinachohusika na kudhibiti ukabaji (SARS) baada ya kukiri kunywa damu ya ng’ombe kabla ya kufanya kazi yake ya uporaji na ukabaji.
Kijana huyu alikiri kutumia damu hiyo kumsaidia kumlinda yeye na kundi lake kila wakitaka kufanya kazi zao za uporaji, vijana hao walikamatwa baada ya damu hiyo ya ng’ombe kushindwa kufanya kazi ambapo mkuu wa kundi hilo alithibitishwa kuuwa kwenye mapigano kati ya kundi la waporaji hao na askari.
Baada ya kijana huyu kuhojiwa alisema ‘ Nashangaa sikuweza kutoroka siku ambayo nilikamatwa na siwezi kukumbuka nimeua watu wangapi wakati nafanya kazi, watu ambao niliwaua ni ambao walikataa kutii amri ambazo nilikuwa nawapa’.
Aliendelea kusema kuwa sababu ya yeye kujiingiza kwenye biashara hizo za ukabaji ilitokana na kulipwa pesa ndogo kutoka kwenye kazi yake ya ulinzi, baada ya muda mfupi aliona kuwa kazi hiyo inampotezea muda kwahiyo akaamua atafute njia nyingine ya kumpa pesa ndio akamtafuta rafiki yake mwenye jina laitwae Umaru Akubaka aliyemtambulisha kwenye kundi hilo la uporaji na ukabaji.
Mtuhumiwa alisema yeye na kundi lake walifanya shughuli zao kwenye mji wa Lagos ambapo walikamatwa baada ya kumuua mlinzi tarehe 11 Mei mwaka huu na akakiri kuwa walipewa silaha na mkuu wa ulinzi wa Omole Estate na kuzitumia kukaba wasafiri wa njia za miguu au kuny’anganya magari kwenye njia panda au gari ambazo zimewekwa kwenye ukingo wa barabara.
Polisi wametoa ripoti na kusema mtuhumiwa huyu atapewa adhabu yake baada ya uchunguzi kumalizika.
via>>Babamzazi.com
Social Plugin