Wananchi wa Tanzania leo wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 15 tangu kufariki kwa Rais wa kwanza na Baba wa Taifa hilo hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwalimu Nyerere alifariki nchini Uingereza alikokuwa amelazwa kwa kusumbuliwa na maradhi ya kansa ya damu.
Alizikwa katika kijiji cha Mwitongo Butiama Kaskazini mwa Tanzania.
Wakati maadhimisho haya ya kitaifa yanafanyika mkoani Tabora, yakiambatana na kuzimwa kwa mwenge wa uhuru, familia ya Mwalimu, muasisi wa Taifa la Tanzania wao wameadhimisha misa ya kumuombea mwalimu anayetajwa kuwa mwenye heri na harakati za kumtangaza mtakatifu zikiendelea.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ambaye atazima mwenge wa uhuru kwani siku ya leo ni kilele cha mbio za mwenge wa uhuru uliokimbizwa katika mikoa 30 nchini Tanzania mwaka huu 2014.