Tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita saa 12 alfajiri ambapo ilidaiwa kuwa Jack alikuwa chumbani na mwanaume huyo ambaye ni mpangaji, wenzake wakipeana maraha.Imedaiwa kuwa, wawili hao walikuwa wakimtegea Ngosha akitoka kwenda katika shughuli zake, Jazira alikuwa akizama katika chumba cha rafiki yake na kufanya mchezo wa kikubwa.
Mume aliyejulikana kwa jina moja la Ngosha, mkazi wa Mabibo jijini Dar, amemfumania rafiki yake aitwaye Jazira akiwa chumbani na mkewe Jack wakiivunja amri ya sita ya Mwenyezi Mungu.
Wapangaji wenziye na Jack wamedai kuwa, mke huyo wa mtu ambaye ana miezi miwili tangu aolewe kutoka mkoani Tabora, amekuwa kero katika nyumba hiyo kwani amekuwa akipiga kelele za kimahaba nyakati za asubuhi ambapo watu wengi wanakuwa wakielekea kazini.
"Hata sisi wanawake tunaoishi nyumba hiyo tuna waume zetu tunawalilia lakini kinachotusikitisha mwenzetu anamlilia Jazira badala ya mumeweambaye anakuwa amekwenda kazini," alisema mmoja wa wapangaji wa nyumba hiyo.
Imeelezwa kuwa, siku hiyo mlinzi wa msikiti alikwenda kumwamsha Ngosha kwenda kusogeza gari lake ili watu wapite na alipofika katika chumba chake, alikuta mlango wa sebuleni ukiwa wazi lakini hakukuwa na mtu, ila chumbani kwake kulisikika redio ikizungumza kwa sauti kubwa.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema, alipofika Ngosha nyumbani na kutonywa kilichotokea alipandwa na hasira na kuangusha varangati kwa rafiki yake lakini baadaye akatulizwa, akamtaka Jazira amlipe shilingi milioni 1.2 ili amuachie mke moja kwa moja.
JAZIRA ANA LAKI 2
Jazira alisema hakuwa na kiasi hicho isipokuwa anaweza kulipa shilingi laki mbili tu, jambo lililomfanya Ngosha kuomba msaada wa askari mgambo na kumpeleka mgoni wake Kituo cha Polisi cha Urafiki kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.