Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAAJABU TANZANIA_MTI ULIOANGUKA MIAKA MITATU ILIYOPITA WANYANYUKA GHAFLA HUKO TABORA,TAZAMA VIDEO HAPA



10447627_721894961214173_1875934379784445685_nPichani ni mti unaodaiwa kunyanyuka ghafla baada ya kuanguka miaka mitatu iliyopitakatika kijiji cha Mfuto kata ya Ufuluma ,ambapo wilaya ya Uyuwi mkoani Tabora.
Katika hali ya kushangaza huku kila mtu akifikiria yake baaya ya juzi huko  mkoani  Tabora, kutokea tukio la aina yake ambapo inaelezwa kuwa mti  aina ya Msufi uliokuwa  umeanguka yapata miaka  mitatu  iliyopita umesimama  ghafla  tena  kwa  sauti  kubwa ya  mrindimo na kuwafanya wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo.

Tukio hilo limetokea  Oktoba 17,mwaka huu,katika kijiji cha Mfuto kata ya Ufuluma katika wilaya ya Uyuwi mkoani Tabora.

 Inaelezwa kuwa mti huo wenye kipenyo cha futi 2 uliinuka na kuwa kama zamani baada ya kutokea upepo mkali katika kijiji hicho.
Wananchi walikusanyika kila  mmoja akitaka kuchukua angalau gome la mti huo  kwa ajili ya  dawa ama kumbukumbu , na haya  ndio maajabu ya Tanzania.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
AU HAPA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com