Aliyeshikilia kipaza sauti ni mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Festo Kang'ombe akitoa taarifa juu ya uchaguzi wa serikali za mitaa katika kikao baraza la madiwani wa manispaa hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo.Kulia kwake ni naibu mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila aliyekuwa mwenyekiti wa kikao hicho(madiwani hawako pichani)-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Akitangaza maeneo mapya ya uchaguzi wa serikali za
mitaa mwaka huu katika manispaa ya Shinyanga,mkurugenzi wa manispaa hiyo Festo Kang’ombe amesema
tayari kanuni za uchaguzi huo zimeshatoka na kilichobaki katika manispaa hiyo ni kupokea vifaa kwa
ajili ya uchaguzi huo unaotarajia kufanyika tarehe 14,Desemba mwaka huu.
Kang’ombe amesema uchaguzi utafanyika katika kata 17 ukihusishwa mitaa 55 badala ya 25 ya chaguzi zilizopita,pia sasa tuna vijiji 19 badala ya 17 vya zamani
na vitongoji 85.
“Leo nimetoa tangazo kuhusu maeneo mapya ya uchaguzi wa serikali za
mitaa mwaka huu,matangazo yapo katika ofisi za kata na manispaa ya Shinyanga,vijiji vilivyofutika ni viwili”.