Mahujaji
zaidi ya milioni mbili wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu jana
wamesimama katika uwanja wa Arafa kutekeleza nguzo kuu ya ibada ya Hija
ambako wameshinda wakiomba dua na kumtaradhia Mola Muumba.
Wageni hao wa Nyumba
ya Mwenyezi Mungu walishinda katika uwanja huo na wamenza kuondoka hapo
baada ya kuzama jua wakielekea Muzdalifa.
Ripoti zinasema kuwa hadi jioni ya jana hakukuripotiwa tukio lolote la kutia wasiwasi.
Mahujai hao watakesha Muzdalifa na
kumdakia Mina katika siku ya kumi ya Dhulhaji kwa ajili ya ibada ya
kumpiga mawe shetani na kuchinja mnyanya wa sadaka.
Serikali ya Saudi Arabia inasema
kuwa karibu Waislamu milioni moja na nusu kutoka nje ya nchi
wanatekeleza ibada ya Hija mwaka huu mbali ya mamia ya maelfu ya
Mahujaji kutoka maeneo mbalimbali ya Saudia kwenyewe.
Social Plugin