Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MASANJA MKANDAMIZAJI NA FID Q WAVUNJA UKIMYA JUU YA SAKATA LA MISS TANZANIA 2014

Miss TZ
Kama ulifuatilia shindano la Miss Tanzania 2014 weekend iliyopita utakua unajua kilichotokea na kinachoongelewa ikiwa ni baada ya baadhi ya watu kupinga au kutoridhishwa na matokeo ya mshindi aliyetangazwa ambae ni Sitti Mtemvu mtoto wa mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu.
Kumekuwepo na malalamiko mengi sana hasa kwenye mitandao ya kijamii ambako zimesambazwa hadi picha zake pamoja na hati za kusafiria, ishu nyingine ikizungumzwa kwamba kuna uwezekano amedanganya umri na elimu yake.
MASANJA AFUNGUKA

MISS TANZANIAAAAAA!!! ...HIVI LUNGENGA UKOJE? ...NILIKUWA NAKUAMINIA SANA.. ...SASA MBONA UNANIANGUSHA BRO! ...HIVI HAYO MANENO WANAYOSEMA HUYASIKIIIII?? ...HIVI UNATAKA MUNGU AKUPE NINI LAKINIII? ...HIVI UNATAKA MPAKA UISIKIE SAUTI YA MUNGU NDO USHTUKE... ...AMKA BRO WAKE UPPPPPPPPPP!! 

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++



Haya ndio aliyoyaandika rapper Fid Q kuhusu malalamiko ya Watanzania yanayoendelea juu ya umri wa mrembo huyu.
Fid Q 1
Fid Q 2
miss TZ 2

WAKATI HUO HUO HABARI ZINASEMA
Kigogo wa RITA aliyetoa cheti kwa mtoto wa mbunge Abbas Mtevu ameanzwa kuchunguzwa kama kweli alifuata taratibu za utoaji wa cheti.

Vikao vilikuwa vikiendelea RITA manispaa ya Temeke kujua kama kweli cheti ni original au cha kupika, ingawa taarifa za ukweli ni kwamba cheti hicho ni original.
Inaonyesha Sitti Mtemvu anamiliki vyeti viwili
1. Kabla ya rita kuanzishwa . Ambacho alizaliwa 1989

2. Kipya kinachooonesha ana miaka 18.

Haki itendeke isiwe ugomvi wa wakurugenzi wa Rhino agency ; wanamtupia msala binti Mtemvu.


HABARI KAMILI IKO HAPA KUHUSU SAKATA HILI

 Kashfa imemwandama Miss Tanzania 2014, Sitti Mtevu baada ya vielelezo mbalimbali kuonyesha kuwa ameghushi umri.
Sitti katika fomu zake alijaza ana miaka 18, kitendo ambacho kimewashtua watu wengi na kuanza kufuatilia taarifa zake na kubaini kuwa kumbe ana miaka 25.
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, mrembo huyo aliyetokea Kanda ya Temeke hakuwa na sifa za kushiriki mashindano kwa vile tayari alishavuka umri uliowekwa kikanuni na waandaaji wa shindano hilo.
Sifa za mshiriki wa Miss Tanzania, anatakiwa awe na umri wa miaka 18 hadi 23, awe raia wa Tanzania, awe hajaolewa, awe na ufahamu wa kutosha wa kujieleza, awe hajazaa, asiwe mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari.
Pia, asiwe ameshiriki mashindano ya Miss Tanzania katika ngazi yoyote zaidi ya mara moja kwa mwaka husika, maana yake hairuhusiwi kushiriki mara mbili katika mwaka mmoja. Lugha inayotumika ni Kiswahili na Kingereza.
Lakini, katika hali ya kushangaza, licha ya mrembo huyo kukiuka masharti hayo, alitangazwa kuwa Miss Tanzania mwaka huu, ushindi ambao umezua mjadala kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiponda ushindi wake na wengine wakienda mbali na kudai mrembo huyo ana mtoto.
Mastaa mbali mbali wame
toa matamko yao kwenye mitandao ya kijamii wakiponda ushindi huo na kuilaumu Kamati ya Miss Tanzania kuvurunda.
Mwanamitindo Martin Kadinda alisema: “Uncle Lundenga nakuheshimu na ninakuamini, lakini katika hili sikuungi mkono.”
Mtayarishaji wa kipindi cha Diaspora, Jestina George alisema:
“Jamani eee uongo kila mtu anadanganya na makosa wote tunafanya mimi bado nawalaumu viongozi wa Miss Tanzania maana naamini asilimia 100 walilijua hili toka mwanzo. Sitti mama pole.”
Akizungumzia suala hilo, mratibu wa Miss Tanzania Hashim Lundenga alisema: “Ni changamoto kubwa, lakini naamini ndio kukua kwa mashindano, mwaka jana na juzi walisema shindano limedoda, mwaka huu wanalizungumzia wiki nzima, acha watu waseme ni upepo tu utapita.”
Meneja wa Redd’s, wadhamini wa mashindano hayoilo, Victoria Kimaro alisema: “Kwa kweli maneno yamekuwa mengi, ya kweli na uongo, lakini naamini mengi ni ya uongo, siku yoyote kuanzia sasa Sitti atazungumza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com