BONDIA Imani Daudi anatarajia kupigan
a na Patrick Amote kutoka kenya kwenye mpambano wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi utakaofanyika katika ukumbi wa musoma bar Tandika siku ya kumbukumbu ya baba wa Taifa Nyerere Day tarehe 14 mwezi huu mpambano huo unaoratibiwa na oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO chini ya Rais wake Yassin Abdallah 'Osthadhi'

lina marengo ya kumkumbuka baba wa taifa katika siku hiyo ya kipekee kabisa kwa nchi yetu ya Tanzania
akizungumza na mwandishi wa habari
hizi Abdallah amesema kuwa kila mwaka wanafanya hivyo kwa ajili ya
kumkumbuka baba wa taifa hili ambaye alipenda michezo mbalimbali bila
ubaguzi wa aina yoyote hile ingawa kwa sasa michezo inabaguliwa kwa
mingine kupewa ufadhili na mingine kupewa kidogo na mingine kunyimwa
kabisa ufadhili
aliongeza kuwa siku hiyo pia kutakuwa
na mipambano mbalimbali ya utangulizi moja likiwa bondia Shomari Milundi
atamenyana na Suma Ninja na mapambano mengine mbalimbali
nae bondia Imani Daudi amejidhatiti
kufanya kweli kwa kumsambalatisha Amote wa kenya ili aendeleze wimbi
lake la ushindi na kuvutia mashabiki zaidi katika mchezo huo wa masumbwi
Social Plugin