Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NI SHIDAAA!! TAZAMA PICHA MATUKIO YA MWENGE WILAYANI KISHAPU NA MAPOKEZI LEO MKOANI TABORA

Hapa ni katika kijiji cha Mayanji wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga ambako jana Oktoba 6,2014 mwenge wa uhuru ulikabidhiwa katika wilaya ya Kishapu ukitokea katika wilaya ya Shinyanga,aliyeshikilia mwenge ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi akaikabidhi mwenge huo kwa mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku(wa kwanza kulia)-Picha na Kadama Malunde

Hapa ni katika shule ya msingi Mayanji katika wilaya ya Kishapu ambako kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu Rachel Stephen Kassanda akifungua mradi wa jiko la gesi kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo mradi ambao ni wazo la mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi kwa kushirikiana na wananchi wake-Picha na Kadama Malunde

Hapa ni Ukenyenge ambako kiongozi wa mbio za mwenge alikabidhi ng'ombe wa maziwa kwa wananchi sambamba na kukabidhi hundi za mikopo kwa wanawake wajasiriamali-Picha na Kadama Malunde

Vijana wakiwa juu ya pikipiki zao katika kijiji cha Mwamashele kata ya Mwamashele wilayani Kishapu ambapo kiongozi wa mwenge mwaka huu Rachel Kassanda alikabidhi pikipiki 21 kwa vijana 21 zinazotokana na mfuko wa jimbo hilo-Picha na Kadama Malunde

 Kiongozi wa mwenge mwaka huu Rachel  Stephen Kassanda akijaribu kuendesha moja ya pikipiki hizo-Picha na Kadama Malunde
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akimtwisha ndoo ya maji  Kiongozi wa mwenge mwaka huu Rachel  Stephen Kassanda baada ya kufungua mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Bubinza katika kata ya Mwamashele-Picha na Kadama Malunde
Hapa ni katika hospitali ya wilaya ya Kishapu ambapo kiongozi wa mwenge mwaka huu aliweka jiwe la msingi katika jengo la wagonjwa wa nje(OPD)-Picha na Kadama Malunde

Kiongozi wa mwenge mwaka huu Rachel  Stephen Kassanda akiweka jiwe la msingi katika kituo cha Mabasi cha wilaya ya Kishapu katika mji wa Mhunze-Picha na Kadama Malunde

Tunaangalia mwenge wa uhuru......-Picha na Kadama Malunde

Kiongozi wa mwenge mwaka huu Rachel  Stephen Kassanda akikabidhi seti ya vyombo kwa akina baba ntilie na mama ntilie katika mji wa Mhunze-Picha na Kadama Malunde

 Ni katika uwanja wa Shirecu mji wa Mhunze viongozi mbalimbali akiwemo mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa wilaya ya Kishapu Boniface Butondo-Picha na Kadama Malunde
Kiongozi wa mwenge mwaka huu Rachel  Stephen Kassanda akikabidhi kombe la Mwenge Cup ambapo mshindi ilikuwa timu ya Mondo Mashariki ambao walipewa kitita cha shilingi milioni 2,washindi wa pili Mondo magharibi waliojinyakulia shilingi milioni 1.5 na mshindi wa tatu Mhunze fc walioondoka na shilingi Milioni 1.-Picha na Kadama Malunde

Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa wilaya ya Kishapu Boniface Butondo akiwasalimia wakazi wa mji wa Mhunze-Picha na Kadama Malunde

TABORA_Wakimbiza mwenge mkoa wa Shinyanga wakiwasili katika eneo la Nata wilaya ya Nzega mkoani Tabora kukabidhi mwenge huo baada ya kuukimbizi siku 6 mkoani humo-Picha na Kadama Malunde

Wa tano kutoka kulia ni mkuu wa mkoa wa Tabora  Fatuma Mwasa akiwa tayari kupokea mwenge wa uhuru leo asubuhi-Picha na Kadama Malunde

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga(kushoto) akiagana na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu Rachel Stephen Kassanda mkoani Tabora-Picha na Kadama Malunde

 Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akikabidhi mwenge wa uhuru baada kukimbizwa siku 6 mkoani humo na kupitia miradi 58 yenye thamani ya shilingi bilioni 7.6-Picha na Kadama Malunde
Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatuma Mwasa(katikati) akipokea mwenge wa uhuru leo mkoani Tabora -Picha na Kadama Malunde

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com