Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amemteua Bwana Lusekelo Mwaseba (pichani) kuwa Naibu Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam, leo, Jumatano, Oktoba Mosi,
2014, na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, imesema kuwa uteuzi
huo unaanza leo.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mwaseba alikuwa Kamishna wa Uchunguzi katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
1 Oktoba, 2014.
Social Plugin