Mshambuliaji
kutoka nchini Ureno Cristiano Ronaldo atarejea tena kwenye uwanja wa
Old Trafford mjini Manchester mwezi ujao imethibitika hivyo.
Kwa
mujibu wa mkataba uliosainiwa na mashirikisho ya soka nchini Ureno
pamoja na Argentina imebainika wazi kwamba mshambuliaji huyo atakuwepo
uwanjani hapo kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya
pande hizo mbili.
Hatua
hiyo huenda ikawatuliza baadhi ya mashabiki wa Man Utd wanaohitaji
kumuona Ronaldo akirejea uwanjani hapo akiwa amevaa jezi ya klabu yao
baada ya kufanya hivyo miaka minane iliyopita.
Kikosi
cha Ureno ambacho kwa sasa kinaongozwa na mshambuliaji huyo kama
nahodha kitacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki katika uwanja wa Old
Trafford Novemba 18 mwaka huu.
Fursa
hiyo itamuwezesha Cristiano Ronaldo kurejea Old Trafford kwa mara ya
pili tangu alipoondoka Man Utd mwaka 2009, na kama itakumbukwa kwa mara
ya kwanza alirejea wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya
miaka miwiwli iliyopita akiwa na Real Madrid.
Social Plugin