|
Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 12 aliyekuwa anasoma katika moja ya shule za msingi katika manispaa ya Shinyanga anayedaiwa kubakwa na baba yake wa kambo tangu mwaka 2011 hadi mwezi huu mwaka huu 2014.Jina na sura tumeficha kwa sababu za kimaadili.Hapa yupo katika ofisi za shirika la AGAPE mjini Shinyanga akisimulia waandishi wa habari kisa kilichompata.Mwanafunzi huyu amekatishwa masomo baada kupata ujauzito hivyo kupoteza haki yake ya elimu.Shirika la lisilo la kiserikali linalojihusisha na utetezi wa haki za watoto na wanawake la AGAPE limejitokeza kumfadhili ili aendelee na masomo yake lakini katika mfumo usio rasmi. |
|
Kulia ni diwani wa viti maalum kupitia CCM bi Marium Nyangaka,kushoto ni mwandishi wa habari gazeti la Mwananchi Suzy Butondo wakiwa kwenye ofisi za AGAPE |
|
Mkurugenzi wa shirika la AGAPE mkoa wa Shinyanga John Myola akizungumza na waandishi wa habariambapo wanalaani kitendo cha mwanafunzi huyo
mwenye umri wa miaka 12 kufanyiwa ukatili huku akitishiwa kuuawa endapo
angesema alivyokuwa anafanyiwa ukatili huo.Alisema kufuatia mwanafunzi huyo kukatishwa masomo kwa
kupewa ujauzito shirika la AGAPE limejitolea kumpatia elimu masafa katika shule
yao ili aweze kupata haki yake ya elimu.
|
|
Kushoto ni mtangazaji radio Faraja fm stereo Steve Kanyefu,akifuatiwa na Marco Maduhu,wa kwanza kulia ni Kadama Malunde mkurugenzi wa malunde1 blog |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com