Ni bora kuwa mwangalifu hasa kuhusu kile unachoahidi watu maana yanaweza ya kukuta kama yaliyomkuta mwanasiasa mmoja nchini Bolivia.
Mwanasiasa huyu Jorge "Tuto" Quiroga, alikuwa mgombea wa urais katika uchaguzi uliokamilika Jumapili iliyopita nchini Bolivia.
Rais huyo wa zamani ambaye pia alikuwa mpinzani mkuu wa Rais Evo Morales alitoa ahadi moja ambayo ikiwa angejua matokeo kabla ya uchaguzi basi asingedhubutu kuitoa.
Ilikua ahadi ambayo haikuwa na busara.
Aliahidi kula saa yake ikiwa kila wabolivia 'sita' kati ya 'kumi' wangempigia kura Rais Morales.
Alikuwa na uhakika sana kuwa Morales asingeweza kushinda uchaguzi kiasi cha kutoa ahadi nyingine ya kutatanisha ya kula tai yake katika mahojiano mengine siku chache zilizofuata.
Na sasa mitandao ya kijamii nchini Bolivia Facebook na Twitter imejaa taarifa za wananchi kumtaka mwanasiasa huyo atimize ahadi zake.
Mwanzo ale saa yake na kisha afuatie ne tai yake.
''Je ni lini ambapo Tuto Quiroga atakula saa yake?'' alihoji mtu mmoja.
Tuffi Aré, mtumiaji maarufu wa Twitter alimhoji bwana Quiroga kabla ya uchaguzi mkuu.
Yeye alituma ujumbe kwa Twitter akisema labda bwana huyo anasubiri matokeo kamili ya uchaguzi ndipo ale saa yake.
Pia alihidi atakula Tai yake na yote hayo yalinakiliwa.
Ingawa watu wengi nchini Bolivia wametoa maoni yao kwenye Twitter na Facebook, wengi wanaomshinikiza mwanasiasa huyo ni wafuasi wa Rais Evo Morales aliyeibuka mshindi wa uchaguzi huo.
via>>BBC