Nyumbani kwa mzee Alley vilio, nyuso za uhuni zilitawala.Wanafunzi hao wawili waliokuwa wanasoma katika shule ya sekondari Uhuru mjini Shinyanga wamefariki dunia wakati wakiogelea kwenye Bwawa la Ning'wa lililopo nje kidogo ya mji wa Shinyanga.-Picha na Kadama Malunde
Wakazi wa Shinyanga wakisindikiza mwili wa marehemu Hussein Alley kwenda katika nyumba yake ya milele jioni ya leo-Picha na Kadama Malunde
Mazishi ya kijana Hussein Alley yamehudhuriwa pia na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga ndugu Khamis Mgeja(mwenye kibaragashia) na katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Shinyanga Emmanuel Mlimandago (kulia kwake na Mgeja)-Picha na Kadama Malunde |
Mwili wa marehemu Hussein Alley ukifikishwa kwenye makaburi ya Nguzo nane jioni hii kwa ajili ya mazishi-Picha na Kadama Malunde |
Mazishi yanaendelea-Picha na Kadama Malunde
Mazishi yanaendelea...pichani ni vumbi la udongo-Picha na Kadama Malunde |
Kaka yake na Hussein Alley,Shaban Alley(wa tatu kutoka kushoto) akiwa eneo la mazishi leo -Picha na Kadama Malunde
Baada ya mazishi ndugu wa marehemu Hussein wakiwa kwenye kaburi(mwenye kanzu ni ndugu Shaaban Alley kaka yake na Hussein Alley)-Picha na Kadama Malunde
Malunde1 blog inawapa pole ndugu jamaa na marafiki wote waliofikwa na msiba.
Mungu azilaze mahali pema peponi roho za marehemu.Amina!!
Social Plugin