TAZAMA PICHA-MATUKIO MBALIMBALI MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2014-WILAYANI KAHAMA MKOA WA SHINYANGA
Sunday, October 05, 2014
HALMASHAURI YA USHETU_Mbio za Mwenge Kahama-Hapa ni katika eneo la Zahanati ta Mwabomba katika halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga.Aliyepo katikati ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru 2014 Rachel Stephen Kassanda aki akifungua zahanati hiyo iliyojengwa na serikali kwa kushirikiana na shirila la AMREF,kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya,kushoto kwake ni mkuu wa polisi wilaya ya Kahama.Mwenge wa uhuru umekimbizwa wilayani Kaham kuanzia Octoba 1-3 mwaka huu katika halmashauri zake tatu za Ushetu,Kahama mji na Msalala na kukabidhiwa wilaya ya Shinyanga Octoba 4,2014-Picha na Kadama Malunde
Jengo la ofisi ya kata ya Saba sabini katika halmashauri ya Ushetu ambayo ilizinduliwa na kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu Rachel Stephen Kassanda-Picha na Kadama Malunde
Hapa ni katika kijiji cha Mseki kata ya Bulungwa ambako viongozi wa mbio za mwenge mwaka huu walitoa ujumbe wa mwenge mwaka huu,kauli mbiu ikisema "Katiba ni sheria kuu ya nchi,jitokeze kupiga kura ya maoni ya katiba mpya"mapambano dhidi ya malaria,UKIMWI,dawa za kulevya na rushwa-Picha na Kadama Malunde
Mmoja wa wakimbiza mwenge Luten Oscar Mlowezi akizungumza na wananchi wa Bulungwa ambapo aliwataka walimu wanaohubiri siasa shuleni waache tabia hiyo na kama kuna mwalimu anapenda siasa aache ualimu.Pia aliwataka wananchi kufanya shughuli za maendeleo badala ya kuendekeza maandamano-Picha na Kadama Malunde
Wakazi wa Bulungwa walijitokeza kuona mwenge wa uhuru kwani eneo hilo kwa mara ya mwisho umepita mwaka 2007 na wengine hwajawahi kabisa kuuona-Picha na Kadama Malunde
Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu akikabidhi cheti kwa mwanafunzi wa shule ya sekondari Mweli iliyopo katika halmashauri ya Msalala,baada ya kuona mradi wa ufugaji nyuki na kuotesha miti katika shule hiyo-Picha na Kadama Malunde
Katika kata ya Ubagwe,wananchi na wanafunzi wakiwa pembezoni mwa barabara kushuhudia mwenge wa uhuru kwani eneo hilo mwenge haujawahi kupita hata siku moja tangu nchi ipate uhuru-Picha na Kadama Malunde
HALMASHAURI YA MJI KAHAMA_Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2014 Rachel Kassanda baada ya kuzindua mradi wa kopa ng'ombe -Lipa ng'ombe eneo la Wigehe/Zongomera.Pichani anamshika ng'ombe wa maziwa mwenye uwezo wa kutoa maziwa lita 16-Picha na Kadama Malunde
Ng'ombe wanaonenepeshwa katika mradi wa ng'ombe eneo la Wigehe ambapo ng'ombe mmoja anakadiriwa kuwa na uzito wa kilo 800 hadi 900-Picha na Kadama Malunde
Wakazi wa Kahama mji wakishika mwenge wa uhuru,anayewapa ni mmoja wa wakimbiza mwenge mwaka huu Yusuph Athman Shesha-Picha na Kadama Malunde
Afisa mahusiano mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo Kahama Dorothy Bikurakule akiwa ameshikilia mwenge wa uhuru baada ya kiongozi wa mbio za mwenge kuzindua barabara ya lami ya Zongomera-Lumelezi-Polisi mjini Kahama,barabara ambayo kwa kiasi kikubwa imetokana na mchango wa mgodi wa Buzwagi uliochangia fedha za ujenzi huo-Picha na Kadama Malunde
Kaimu meneja mkuu mgodi wa dhahabu wa Buzwagi Amos John akiwa ameshikilia mwenge wa uhuru katika eneo la Nyihogo mjini Kahama baada ya uzinduzi wa moja ya barabara mjini Kahama wakati wa mbio za mwenge wilayani Kahama-Picha na Kadama Malunde
Kahama mjini ilikuwa full shangwe,wananchi wakikimbiza mwenge huku nyimbo za "Mwenge ooo mwenge mbio mbio,tunaukimbiza mbio mbio......"-Picha na Kadama Malunde
Hapa ni katika kituo cha polisi Kahama ambapo kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu alifungua jengo la ofisi ya upelelezi -Picha na Kadama Malunde
Kushoto ni mkuu wa polisi wilaya ya Kahama akikabidhi taarifa ya ujenzi wa jengo hilo-Picha na Kadama Malunde
Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu Rachel Stephen Kassanda akiteketeza bangi katika kituo cha polisi Kahama mjini-Picha na Kadama Malunde
Wanafunzi wa shule ya sekondari Anderlek Ridges ya mjini Kahama wakishika mwenge wa uhuru-Picha na Kadama Malunde
Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu Rachel Stephen Kassanda akisalimiana vijana wa skauti katik shule ya sekondari Anderlek ridges-Picha na Kadama Malunde
Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu Rachel Stephen Kassanda akipanda mti katika shule hiyo,ambayo ina klabu ya wanafunzi ya mazingira ambao kupanda miti,huotesha na kuuza miti na kufanya shughuli mbalimbali za utunzaji mazingira ili yawe rafiki kwa binadamu-Picha na Kadama Malunde
Ndani ya eneo la shule ya sekondari Anderlek ridges,wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa malunde1 blog,ndugu Kadama Malunde
Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu Rachel Stephen Kassanda akifanya usafi katika shule hiyo na kuweka uchafu katika moja ya mapipa 100 ya kuwekea taka yaliyotolewa na mgodi wa Bulyankulu-Picha na Kadama Malunde
Ebwana eeee noma sana,mambo ya mwenge eneo la Kagongwa mji Kahama-Picha na Kadama Malunde
Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu Rachel Stephen Kassanda baada ya kufungua soko la jipya la Namanga-Nyihogo mjini Kahama-Picha na Kadama Malunde
HALMASHAURI YA MSALALA-Hapa ni katika eneo la mgodi wa Umoja Plant unaohusika na uchenjuaji wa dhahabu katika kijiji cha Nundu kata ya Chela halmashauri ya Msalala ambako kuliwekwa jiwe la msingi katika ofisi za mgodi-Picha na Kadama Malunde
Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu Rachel Stephen Kassanda na msafara wake wakiangalia namna uchenjuaji wa dhahabu unavyofanyika katika mgodi huo ambao hadi sasa umewapatia ajira vijana 48-Picha na Kadama Malunde
Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu Rachel Stephen Kassanda akiwa ndani ya ghala la kuhifadhia chakula katika kijiji cha Malito halmashauri ya Msalala,akifurahia jambo na mdiwani wa halmashauri hiyo-Picha na Kadama Malunde
Kaka mkuu wa shule ya msingi Malito akiwa ameshikilia mwenge wa uhuru-Picha na Kadama Malunde
Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu Rachel Stephen Kassanda akiwa amebeba mtoto aliyezaliwa kwa njia ya upasuaji katika kituo cha afya cha Lunguya halmashauri ya Msalala baada ya kufungua jengo la upasuaji na kuona shughuli za upasuaji katika kituo hicho-Picha na Kadama Malunde. Mpenzi msomaji wa blog hii,Tutakuletea pia picha za mbio za mwenge katika wilaya ya Shinyanga,ambazo zimeanza Octoba 4 na kufikia tamati Octoba 5,kabla ya mwenge kukabidhiwa wilayani Kishapu tarehe 6,2014,endelea kutembelea Malunde1 blog,Fahari ya Shinyanga KUONA PICHA ZA MAPOKEZI YA MWENGE SHINYANGA UKITOKEA GEITA,BONYEZA MANENO HAYA
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin