Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Geita Joseph Msukuma
Na mwandishi maalum kutoka Geita
|
Siku chache tu baada ya vyombo vya habari kuandika habari kuhusu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Geita Joseph Msukuma kuhamasisha wananchi kurudi na kuvamia eneo la mwekezaji Majaliwa Maziku mwenye leseni lililoko katika kijiji cha Nyantorotoro wilayani Geita mkoani humo,sasa mwenyekiti huyo ameibuka na kuanza kuwatishia waandishi wa habari walioripoti habari hizo.
Akiongea na waandishi wa habari kwa kuwapigia simu mmoja baada ya mwingine huku akifoka amesema kuwa waandishi wote walioripoti habari hizo atahakikisha anawaburuza mahakamani ili washike adabu kwani yeye anawatetea wananchi wake.
Msukuma alisema kuwa waandishi hao wamekuwa wakitumiwa na mkuu wa ilawya ya Geita Omary Mangochie kwa kuandika mambo ambayo yanamchafua.
"Nyinyi mnatumiwa na mkuu wa wilaya kwa kunichafua nitawaburuza mahakamani nione kama huyo DC atakuja kuwatoa kwani ndiye anayewatuma kuniandika",alisema Msukuma.
Hivi karibuni Msukuma aliwahamasisha wananchi wasiokuwa na leseni kwenda kuvamia eneo la mwekezaji na kuanza kufanya fujo kwa wafanyakazi wa muwekezaji huyo ambapo walitimkia kusik julikana na jeshi la polisi Wilaya ya Geita likingilia kati sakata hilo.
Habari kutoka Geita zinasema mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Geita amekuwa na mambo ya kuwapinga viongozi wenzake kwa kuwakataza wananchi kufanya mambo ya kuwaletea maendeao na kutumia mabavu kwa tiketi ya chama tawala.
MSIKILIZE HAPA CHINI MWENYEKITI HUYU AKIFOKEA MMOJA WA WAANDISHI WA HABARI WA GEITA
Social Plugin