Mwanasoka wa kibrazil David Luiz jana usiku alikuwa mchezaji wa kwanza kuifunga goli FC Barcelona katika msimu mpya wa soka barani ulaya.
Luiz alifunga goli hilo katika dakika ya 11 ya mchezo wa Champions League kati ya klabu PSG dhidi ya Barca.
Mchezo uliopigwa kwenye dimba la Stade de France na kuhudhuriwa na mastaa kama Rais wa zamani wa nchi hiyo Sarkozy, David Beckham na rapa Jay Z pamoja na mkewe Beyonce.
Matokeo ya mchezo huo ni ushindi wa 3-2 kwa PSG dhidi ya kikosi cha Luis Enrique.
Lionel Messi na Neymar walifunga magoli ya Barca huku Matuidi na Verrati wakihitimisha kipigo hicho cha kwanza cha Barcelona katika
Michuano yote ya msimu huu.
Social Plugin