Waumini wa kanisa la Anglikana Wilaya ya Nyamagana Mwanza
walisimamisha kwa muda shughuli za ibada kanisani hapo baada ya kutokea
vurugu kubwa.
Vurugu hizo zilitokea baada ya baadhi ya waumini hao kumtuhumu Askofu
wa kanisa hilo Boniface Kwangu kwamba ni mmoja wa wafuasi wa kundi la
Freemasons na hufanya kazi za kundi hilo.
Mmoja wa waumini wa kanisa hilo Shadrack Lazaro alitoa
tamko la jinsi
askofu wao anavyofanya kazi na kundi la Freemason ndipo waumini
walipomvamia na kumtoa nje ya kanisa kwa nguvu na kusababisha vurugu
kubwa.
Muumini huyo alisema pamoja na sababu kadhaa za kumkataa askofu huyo
pia hawaridhishwi na tabia yake ikiwemo kutaka kubomoa sakafu akidai
kuna Hirizi imefichwa na baadhi ya waumini wake kanisani hapo.
Social Plugin