Kama tulivyoawaahidi kuwaletea simulizi mbalimbali kuhusu kanda ya Ziwa Victoria,kupitia ukurasa/kipengele chetu kipya cha" UTAMADUNI LAKE ZONE",angalia juu kwenye blog,kila siku za Jumamosi ,leo Malunde1 blog inakuletea sehemu ya TANO ya simulizi ya kusisimua kuhusu Gamboshi
SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU GAMBOSHI SEHEMU YA5
Mtunzi; Timotheo Mathias
MAZINGIRA; Shinyanga vijijini.
Simu yake-0765676242(WhatsApp)
timotheomathias0@gmail.com
Maana ya maneno yaliyotumika kwenye simulizi
-GAMBOSHI ni makazi au eneo linalotumika kuhifadhia misukule.
-MSUKULE ni mtu aliyechukuliwa kwa njia ya kishirikina (kichawi) akiwa mzima (hai), lakini kwa upeo wa kawaida ni dhahiri kuwa amekufa
Ilipoishia...........................
Mkuu
alisema "kijana una nyota kali sana haijawahi kutokea kwa mtu nimemuua
aje apone?!! Kama ulivyofanya wewe , sasa basi nitakachokuambia naomba
ufanye".
Mti
niliusogelea na kujitemea mate mkononi na kuishika shoka kisawa sawa
nikainyanyua kwa nguvu zangu zote na kuliachia kwenye mti.
Duh!! kabla shoka halijatua nilishaanga kuona sura ya mama wakati nilimuacha nyumbani.
Endelea...........................
Nilipoiona sura ya mama shoka niliizuia na kuiachia chini na kukaa chini ya mti huo.
Nikiwa nimekaa chini nilianza kuwaza kilichonitokea kwa muda huo mfupi, kwani nilikumbuka kuna siku ambayo msukule aliagizwa kukata mti na mti uligeuka kuwa mama yake lakini yeye aliukata kutokana na shinikizo la mkuu.
Baada ya siku moja msukule alipelekwa nyumbani ili kushuhudia mazishi ya mama yake na mimi nilikuwa mojawapo ya msukule tulioenda kushuhudia mazishi hayo.
Baada ya kufika tulikuta watu wakilia wengine wakiwa wamezimia baada ya marehemu kufa kwa kukatika tu, wakati jana yake alikuwa mzima.

Kwa upande wetu sisi haikuwa rahisi wao kutuona hata kutusikia maana tulikuwa tumepaka dawa machoni na mwili mzima.
Tulishuhudia mazishi yakifanyika huku wakiwa wanazika gogo na mwili wa marehemu kuuacha ndani ya nyumba ukiwa hai.
Tulishuhudia mazishi yakifanyika huku wakiwa wanazika gogo na mwili wa marehemu kuuacha ndani ya nyumba ukiwa hai.
Walipomaliza kuzika Gogo,tuliingia ndani ya nyumba ili kumchukua mtu wetu, tulipoingia ndani bibi tuliyeenda naye alimuita marehemu jina lake na kuitika.
Baada ya hapo alichomoa fimbo yake aliyokuwa ameichomeka kiunoni na kumpigia mgongoni kisha kumshika mkono na kuanza kutoka naye nje.
Wakati tunatoka nje tukiwa na mtu wetu mama mmoja alituangalia sana mpaka tukahisi kama ametugundua na anatuona.

Kiongozi wetu ambaye ni bibi alisema huyu mbona anatuangalia sana? "Hebu ngoja tuhakikishe kama kweli anatuona".
Bibi alinyanyua mkono wake juu, ghafla mshale ulitua mkononi mwake na tukashuhudia fisi mkubwa wa madoa madoa meusi na meupe, mbele yetu kama kawaida yake mbele mrefu nyuma mfupi.
Fisi huyo alikuja kwa kasi ya ajabu hadi tulipokuwa tumesimama kisha akafunga breki huku akisindikizwa na vumbi la kutosha nyuma yake.
Fisi huyo alikuja kwa kasi ya ajabu hadi tulipokuwa tumesimama kisha akafunga breki huku akisindikizwa na vumbi la kutosha nyuma yake.
Bibi alipanda juu ya fisi na kushikilia vizuri mshale wake na kumwamru fisi aondoke kwa kasi huku fisi akimlenga yule mama tuliyehisi anatuona.
Baada ya yule mama tuliyehisi anatuona kuona fisi anakuja anaenda upande wake huku akilengwa ,alianza kupiga kelele huku akikimbia ovyo na kuwafanya watu waliokuwepo kwenye mazishi wakibaki midomo wazi wasijue kilichotokea huku wakimshangaa.

Bibi aliweza kumpata na kumrushia dawa iliyomfanya awe bubu na kushindwa kuwaelezea alichokiona.
Bibi alirudi na wote tuliweza kuondoka kuelekea kambi, lakini huyo mama tuliyemchukua msibani alikakaa siku tatu tu na siku ya nne alichinjwa na kuliwa nyama.
Kuna siku nikiwa nimekaa nimejiinamia nikiwaza yote yaliyotokea mkuu wa wachawi alinifuata na kunishika mkono na wote tukaanza kurudi kambini.
Tulipofika Sheila aliitwa na bibi mmoja pia na yeye aliitwa kwa mkuu, mkuu alimwambia bibi kuwa mwezi ujao ni sikukuu itakayofanyika nchini Nigeria, na huko zinahitajika nyama laini kama wanafunzi wa shule za msingi na baadhi ya walimu wao.
Nimekuchagulia vijana shupavu na imara utawatumia katika mashule huko vijijini kuleta wanafunzi.
Mkuu alipomaliza alitukabidhi mabegi yaliyosheheni pipi, biskuti na hela za sarafu, tayari kwa safari kwenda kuleta roho za watu kama tulivyoagizwa.
Mkuu alipomaliza alitukabidhi mabegi yaliyosheheni pipi, biskuti na hela za sarafu, tayari kwa safari kwenda kuleta roho za watu kama tulivyoagizwa.
Itaendelea sehemu ya 6 wiki ijayo Jumamosi kupitia www.malunde1.blogspot.com
Social Plugin