Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Utamaduni Lake Zone_ SEHEMU YA PILI-SIMULIZI YA KUTISHA KUHUSU "GAMBOSHI"


Kama tulivyoawaahidi kuwaletea simulizi mbalimbali kuhusu kanda ya Ziwa Victoria,kupitia ukurasa/kipengele chetu kipya cha" UTAMADUNI LAKE ZONE",angalia juu kwenye blog,kila siku za Jumamosi ,leo Malunde1 blog inakuletea sehemu ya pili ya simulizi ya Kusisimua kuhusu Gamboshi


SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU GAMBOSHI SEHEMU YA 2


Mtunzi; Timotheo Mathias
Simu yake-0765676242

Maana ya maneno yaliyotumika kwenye simulizi

-GAMBOSHI ni makazi au eneo linalotumika kuhifadhia misukule.

-MSUKULE‬ ni mtu aliyechukuliwa kwa njia ya kishirikina (kichawi) akiwa mzima (hai), lakini kwa upeo wa kawaida ni dhahiri kuwa amekufa.

Sehemu ya 1 ilipoishia..........

Nilikuja kuzinduka nikiwa na makovu mwili mzima na kutazama pembeni yangu nilikuta joka kubwa likiwa na vichwa vinne na kila kichwa kilikuwa na mapembe mawili.



Endelea...............
Kulingana na uchovu niliokuwa nao sikuweza kufanya chochote nilibaki nikishangaa nikiwa sina hata nguvu za kuweza kuinuka na kukimbia.




Ghafla alitokea babu ambaye alikuwa mnene sana akiwa mkononi ameshikilia kibuyu sikujua cha nini, alisogea mpaka nilipokaa ,aliponisogelea niliweza kushuhudia kwa macho yangu joka likigeuka na kuwa pete nyeupe. 


Babu aliisogelea ile pete na kutamka maneno ambayo sikuweza kuyafahamu baadaye na kuichukua ile pete.

Nikiwa nimekaa babu aliniamrisha niinuke, nilishangaa sana maana sikuweza kujua nguvu nimepata wapi?.

 Babu alininyoshea kidole chake cha kulia na kusema "kijana mwisho wa maisha yako ulikuwa umefika lakini kulingana na nyota yako nzuri ndiYo maana ni mzima na upo hapa nishukuru mimi maana waliokupeleka walikuacha peke yako.

Sasa basi kuanzia sasa utakuwa bega kwa bega na mimi, nitakusaidia ,nitahakikisha unarudi uraiani kwa wazazi wako, ukaendelee na masomo yako. 

Chukua hii pete usijaribu kuitupa hata kuvulishwa na mtu wa aina yoyote". 

Nikiwa nimesimama babu alipotea ghafla na baada ya muda mfupi ,yule mama niliyekuwa naye hospitali ,alikuja .lakini alipofika karibu yangu na kuiona pete niliyopewa aliitazama kisha akafyonza kwa dharau.

Sikujua anamaanisha nini. 

Alinishika mkono na kuniamuru nifumbe macho,baada ya kama sekunde 30 aliniambia nifumbue, sikuweza kutambua maeneo tuliyofikia, kulikuwa na nyumba moja.

 Mama aliniambia nimfuate kwa nyuma mpaka mlangoni mwa nyumba tuliyofikia, tulipokaribia tulisimama kwa muda mfupi, baadaye mama mwingine alitua sehemu tuliyokuwepo.

Wakasalimiana, wote wakafurahi, sikujua kipi kilichotupeleka kwenye híi nyumba tena usiku!. 

Mama tuliyekuja naye alinisogelea na kuniambia tunaingia humu ndani kuchukua watu wakatusaidie kulima usiku wa leo baadae watarudi, nikamjibu sawa. 

Tukiwa watatu kwa pamoja tulisogea karibu na mlango,yule mama tuliyekuja naye alisema tukae pembeni aweze kufungua mlango.

 Alisogea karibu na mlango, aliposogea aliushika mlango pande zote nne akarudi kama hatua mbili nyuma, akageuka na kuvua sketi yake akainama. 

Mlango ulianza kufunguka taratibu bila mtu yeyote kujua na alipohakikisha umefunguka aliinuka na kuvuta sketi yake na kutuita kwa ishara ya mkono kwa pamoja.

 Wote tuliingia ndani ya nyumba tukapitiliza hadi chumbani ,tulipofika tulikuta watu watatu wamelala kitandani ,sikujua ni jinsia gani?

 Mama alisogea kwenye kona ya chumba akasimama na kunyosha mkono wake sehemu ya kitanda, niliona mtu mmoja wa kiume (pande la jamaa) akiinuka taratibu na kuufuata mkono wa mama ulipo. 



Alipofika alimshika mkono na kutoka naye nje ya nyumba, tulipofika nje ,alinikabidhi na kuniambia nimpeleke akalime nikiambatana mama aliyekuja peke yake atanitangulia mbele yangu nikiwa mimi nimebebwa mgongoni na jamaa tuliyemchukua. 


Tukiendelea na safari ya kwenda shambani ghafla nilikia kishindo kikubwa pembeni yangu nikatazama na kuona likitokea vumbi likiambatana na kimbunga, upepo mkali ulivuma hadi tulipo na kumshuudia mama aliyekuwa akiniongoza njia akianguka chini na kuanza kutoa mapovu mdomoni hatimaye aliaga dunia.



Nilibaki nikishangaa mithili ya barafu kwenye friji, nikiwa natafakari, ghafla Babu alinitokea mbele yangu akiwa anahema kwa nguvu na kwa kutisha mpaka nilimuogopa. 


Alinyanyua mkono wake wa kulia akiwa ameshikilia mkia wa ng'ombe na kunisonta  kidole akisema "nimekupa pete ili uweze kujiokoa na kuwaokoa walio hatarini lakin leo hii umeanza kuwatumikisha watu wasio na hatia!!!!?? Unabebwa mgongoni unaona raaaahaaaaa!!!? Pumbavuuuuuu!!!!? mkubwa shuka mgongoni? na umurudishe kwake fanya haraka?". 

Kabla sijashuka Babu alipotea ghafla, baada ya muda mama niliyemuacha nyuma alikuja na kuniangalia kwa kunipandisha na kunishuka, akaniuliuza mwenzako yuko wapi? 

Niligeuka ili niweze kumuonyesha alipoangukia na kufa lakini nilishangaa kutokuuona mwili wake wakati amekufa muda si mrefu!, nilibaki nikishangaa mwili umeenda wapi? Lakin sikupata jibu.



Mama aliniamuru nifumbe macho baada muda nikafumbua, nilikuwa sehemu ya kambi nikiwa na misukule wenzangu walioonekana kunishangaa sana mpaka viongozi wa wachawi hasa pete niliyokuwa nimevaa kwenye kidole changu.


 Tukiwa tumepumzika, misukule kulingana na kwamba hakuna muda wa kunyoa nywele zilirefuka kupita kiasi, wengine wakijaribu kukumbushia michezo waliokuwa wakiipenda enzi za uhai wao, pia wengine walikuwa wakisukana lakini mimi nilikaa pembeni na Sheila tukiwa tunabadilishana mawazo. 

Baada ya muda msukule mmoja alitumwa kunifuata nilipokuwa nimekaa na kuniambia ninaitwa na mkuu wa wachawi.

Niliinuka na kuelekea sehemu alipokuwa amekaa nilipofika aliniangalia sana hasa sehemu ya pete ilipokuwa. 

Alipomaliza alitabasamu na kusema "Kijana naona sasa umekuwa na unajiona sana mpaka inafikia mahala unaua watu wangu!!!? Sasa basi kulingana na ushenzi ulionifanyia nakupa kazi ya kunitengezea mafuta lita 5 ya mtoto mchanga utasaidiana na watu wangu nitakaokupa, kazi hiyo kufikia kesho uwe umeshamaliza",aliniagiza mkuu wa wachawi.

 Niliondoka na kuelekea sehemu niliyokuwa nimekaa na Sheila, nikiwa natafakari mtihani niliopewa Sheila aliniuliza vipi kuna tatizo? 

Nilimjibu ndiyo kuna tatizo, nimeambiwa nitengeneze mafuta lita 5 ya mtoto mchanga. 

Sheila alisema mbona hapa gambosi kitu cha kawaida sana maana tunaishi kwa mafuta ya watoto wachanga.

Nilimuuliza kivipi? Sheila alisema mtoto mchanga hasa yule hajatimiza miezi tisa akiwa tumboni mwa mama yake huchukuliwa na kupikwa maana viungo vyake bado vilaini huyeyuka na kuwa mafuta.

 Mafuta hayo huchukuliwa, na hayo mafuta hutumika kwa kupaka sehemu za macho na binadamu wa kawaida hawakuoni.

 Nilimuuliza je, watoto hao wachanga hutoka wapi?

 Sheila alinijibu hutoka kwa mama viongozi wa wachawi kila baada ya miaka 10 kila mama anatoa mtoto, pia wengine huchukuliwa kwenye hospitali kwa miujiza pindi wanapomaliza kuzaliwa tu!.



Tukiwa kwenye mazungumzo na Sheila ,mama mmoja alikuja kunichukua na kwenda sehemu husika ya kupikia watoto, nilikuta moto mkali ukiwaka huku juu yake kuna sufuria lililo chemka mpaka linakuwa jekundu. 


Mama huyo aliniletea kitoto kichanga kikiwa hai na kuniamuru nikitupie ndani ya sufuria harafu nianze kukaanga mpaka nihakikishe yamekuwa mafuta ndani ya sufuria.

ITAENDELEA JUMAMOSI IJAYO KUPITIA www.malunde1.blogspot.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com