SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU GAMBOSHI SEHEMU YA 4
Mtunzi; Timotheo Mathias
Simu yake-0765676242(WhatsApp)
Maana ya maneno yaliyotumika kwenye simulizi
-GAMBOSHI ni makazi au eneo linalotumika kuhifadhia misukule.
-MSUKULE ni mtu aliyechukuliwa kwa njia ya kishirikina (kichawi) akiwa mzima (hai), lakini kwa upeo wa kawaida ni dhahiri kuwa amekufa
Ilipoishia...........................
Nilibebwa na kupelekwa kusikojulikana maana nilikuwa sioni, macho yangu yaliziba na kuwa kipofu.
Nilipelekwa sehemu ambayo nilihisi kama nimeingizwa kwenye handaki.
Nilipofikishwa hapo ghafla nilianza kuhisi joto na mwili mzima kuniwasha.
Mara nikaanza kusikia harufu ya damu ya binadamu na kusikika sauti ikisema omba sara ya mwisho.
Kabla sauti haijamalizika nilisikia kishindo kikitua mbele yangu, baada ya muda kidogo nilipokea kofi takatifu la usoni ambalo lilinipeleka mpaka chini ambapo niliweza kuangukia kwenye moto.
Endelea....................
Baada ya kupokea kofi takatifu nilipoteza fahamu sikuweza tena kujitambua kutokana na maumivu ya moto niliyoyapata.
Nilikuja kuzinduka nipo chini ya mti nikiwa na Sheila akiwa ananihudumia huku mwili wangu ukiwa umepakwa dawa za majani mabichi yaliyopondwa hasa sehemu niliyoungua moto.
Nikiwa najisikia maumivu nilimtazama Sheila kwa huruma na kunyanyua mkono wangu wa kuume, naye Sheila aliupokea.
Nikamuuliza "Nimefikaje hapa? Na wewe umenionaje?"
Aliuchukua mkono wangu taratibu!!!!!! Huku machozi yakimtiririka na kisha alinisogelea na kunikumbatia huku akitabasamu na kusema...
"Timothy amini usiamini nimekuhudumia siku tano bila ya wewe kujitambua siamini leo umezinduka!!" .
Sheila alipomaliza kunieleza alinikumbatia tena kwa furaha, nikamuuliza hapa nimefikaje??
Sheila alinyamaza kwa muda kisha akasema
"Ni stori ndefu sana, siku moja nilikuwa nimekaa na misukule wenzangu babu mmoja alinitokea na kuniuliza Timothy unamfahamu???
Nikamjibu ndiyo namfahamu akaniambia leo ni siku ya pili amepoteza fahamu tena alienda kutupwa baada ya kugundulika kuwa alikuwa amekufa, nilishtuka na kumuuliza yupo wapi?????
Babu alinichukua na kunileta mpaka hapa ulipo na kuanza kukata kata majani na kuyaloweka mwenye maji na mengine nikakupaka mwilini mwako".
Wakati Sheila anaendelea kunisimulia ghafla nyoka mkubwa alikuja sehemu tulipokuwa tumekaa na Sheila.
Nyoka alipanua mdomo wake na kunitemea mate mwili mzima, nilipiga kelele kutokana na maumivu niliyokuwa nayapata, ghafla nilipata nguvu na kunyanyuka na kukimbia huku nikiendelea kupiga kelele.
Ghafla mbele yangu Babu alitokea na kuanza kunicheka, nilipogeuka nyuma nyoka sikumuona tena.
Babu nilimuuliza nyoka yupo wapi?
Babu akatabasamu na kusema ina mpaka sasa hujanizoea tu????.
Babu akasema sikia kijana mpaka kufikia hapo nimetumia nguvu zangu binafsi, kwanza macho yako nimeyatengeneza kwa kutoa upofu uliokuwa umepewa na kisha kumleta Sheila aje akuhudumie.
Babu nilimuuliza,mbona pete yangu siioni?
Babu akajibu pete niliichukua kwa sababu nilihofia mkuu wa wachawi angeichukua maana nguvu alizokuja nazo sio za kawaida.
Wakati naongea na Babu,Sheila alikuwa amesogea karibu yangu na yote aliyokuwa anayasema Babu aliyasikia.
Ghafla kilitokea kimbunga kilichoambatana na upepo mkali na vumbi, baada ya muda Babu alinishika mkono wa kushoto na kunivalisha pete.
Baada ya muda babu alipotea na kutoweka kimiujiza.
Dakika chache mkuu wa wachawi alitokea mbele yetu na kunyanyua mkono wake huku akitusonta kidole, tulijikuta tumefika kambini.
Kama kawaida tukajichanganya na misukule wenzetu na stories zikaanza kuchukua nafasi yake na masela (misukule) ambao ni wageni bado ndimi zao hazijakatwa.
Nilishangaa kumuona mkuu wa wachawi akija sehemu tuliyokuwa tumekaa na moja kwa moja mpaka sehemu nilipokuwa nimekaa akanishika mkono na kuondoka naye.
tulisimama.
Mkuu alisema "kijana una nyota kali sana haijawahi kutokea kwa mtu nimemuua aje apone?!! Kama ulivyofanya wewe , sasa basi nitakachokuambia naomba ufanye".
Babu alinyoosha mkono wake na shoka kali likatua mkononi mwake na kuniamuru nichukue shoka.
Shoka nillilichukua nikalishikilia. Mkuu aliniambia nigeuke nyuma yangu na kuniamuru niukate mti ambao tulikuwa tumesimama nikamjibu kwa kujiamini HAKUNA TABU MKUU!!!!!!!!!!!!!!!!.
Mti niliusogelea na kujitemea mate mkononi na kuishika shoka kisawa sawa nikainyanyua kwa nguvu zangu zote na kuliachia kwenye mti.
Duh!! kabla shoka halijatua nilishaanga kuona sura ya mama wakati nilimuacha nyumbani.
Itaendelea sehemu ya 5 wiki ijayo Jumamosi kupitia www.malunde1.blogspot.com
Social Plugin