Mwanadada Moza Kassim mwanafunzi wa chuo cha Uhasibu Tawi la Singida,
Inadaiwa kuwa usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi iliyopita mkoani Singida,
Alijibizana na mpenzi wake ambaye eti aligundua kuwa ana mpenzi mwingine na katika vuta ni kuvute hawakufikia muafaka ndipo mwanadada akamwambia mpenzi wake kuwa anajichoma kisu mwanaume akajua ni utani akamjibu huwezi,
Mwanadada akamwambia kwa mara ya pili kisha Moza akajipiga kisu tumboni karibu na kiuno hali yake ikawa mbaya na kuanza kuchuruzika damu.
Ikabidi rafiki zao waliokuwa karibu wakamkimbiza hospitali ya mkoa na jana alihamishwa hospitalini hapo na mwanadada huyo yupo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi, na kwa mujibu wa sheria Moza ana kesi ya kujibu.
Social Plugin